Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe.Mallallah Mubarak Alameri akiongea katika kongamano la kibiashara, kati ya wafanyabiashara kutoka Dubai na Tanzania, lililofanyika leo hapa Dar es Salaam. Aambapo Kampuni ya simu za mikononi ya ZANTEL ni mmoja kati ya wadhamini walioweza kufanikisha mkutano huo.
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Dubai Exports Eng. Saed Al Awadi akielezea jinsi kampuni yake inavyofanya na amepanga kuja kuwekeza nchini Tanzania.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa akiongea machache katika kongamano hilo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdalah Kigoda, nae aliongea machache. 
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mary M. Nagu ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea machache kwa niaba ya serikali.
 Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe.Mallallah Mubarak Alameri akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa  katika kongamano la kibiashara, kati ya wafanyabiashara kutoka Dubai na Tanzania, lililofanyika leo hapa Dar es Salaam.
 Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini kongamano la kibiashara, lililowakutanisha wafanyabiashara kutoka Dubai na Tanzania. 
 Meza kuu wakifuatilia kwa makini.
 Wageni waalikwa walivyokuwa wamejaa.
 Wageni wakiwa wamejaa kila kona.



 Zantel nao wakiwa wamesambaza mabango yao kila kona.
 Wakisaini mkataba na serikali.
 Wakibadilishana mkataba.
 Waziri Marry Nagu akipokeza zawadi yake.
Waziri Abdallah Kigoda nae alipewa zawadi yake.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya ZANTEL, ni mmojawapo wa wadhamini wa kongamano la kibiashara, kati ya wafanyabiashara kutoka Dubai na Tanzania, lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Dubai na Tanzania ili kujadili fursa mbalimbali za kibiashara, na hivyo kukuza mahusiano kati ya pande hizo mbili.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wageni zaidi ya 40 kutoka makampuni makubwa kama Nida Textiles, Micro Automation Industries (MAI), Century Mechanical Systems (CMS), Al Hussain Trading, Corodex, Bristol Fire, na Al Yas Gate.

Akizungumza afisa Biashara mkuu wa ZANTEL bwana Ahmed Mokhles alisema kuwa umuhimu wa Zantel kushiriki katika kongamano hilo,"Tunafuraha kuwa kampuni pekee ya simu kushiriki kuwaleta wafanyabiashara hawa ambayo itakuwa fursa ya kipekee kwa watanzania kubadilishana mawazo na wafanyabiashara wenzao’

Kongamano hilo pia limehudhuriwa na wadau mablimbali kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania, wataalamu kutoka sekta mbalimbali kama afya, nishati na kadhalika.

Dhumuni kuu la Kongamano hilo ni kuzipa pande zote mbili, Tanzania na Dubai, kutambua fursa za kibiashara lakini pia kuimarisha mahusiano kati ya pande hizi mbili.

"Kama kampuni ya simu ambayo pia inatoa huduma za kipekee kwa makampuni ya kibiashara, kuwaleta wafanyabiashara hawa kutasaidia biashara hizo zizidi kukua kwa kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara wengine’’ anasisitiza Mokhles.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: