Wilaya Afisa Ardhi Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari (mwemnye miwani kulia) akitoa maelezo juu ya ramani ya shamba 296 lililopo Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambalo lina mgogoro baada ya Mwekezaji wa Kizungu wa kudaiwa kuvamia mashamba ya wananchi na kufunga njia inayounganisha kitongoji cha Kinyebnze na mwanga kijijini Kipera. Kulia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha mwanga na katikati yao ni Mwanakijiji Mroki Mroki.
Mafisa wa ardhi Wilaya ya mvomero wakiwa katika uhakiki wa mipaka hiyo kijijini hapo jana.
 Wataalam wa upimaji wakiwa kazini
Akina mama na watoto wakifuatilia zoezio hilo.
Afisa mtendaji wa kata ya Mlali, Said Said Mdume akizungumza na maafisa ardhi na wananchi wa Kinyenze baada ya zoezi la upimaji kusitishwa kufuatia wananchi kutaka zoezi hilo lifuate mchoro uliopo unaonesha mpaka wa shamba hilo ni barabara ya waenda kwa miguu na lipo mbali na mto Kinyenze na sio kama ilivyo pimwa na kuvuka mto. 

Zoezi hilo liliamuliwa kuendelea leo na kupima kipande kilicho na mgogoro pekee. hata hivyo uchunguzi uliofanywa na father Kidevu Blog umebaini kuwa Umiliki wa mzungu huyo katika shmba hilo si halali kufuatia Uongozi wa kijiji kudai kuwa haukuwahi kutoa Muktasari kwaajili ya kupata hati ambayo ilishamalizika. Picha/Mroki Mroki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: