Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma Keseja baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo uliokuwa ni wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza.
Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu, Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari. Picha/FullShange Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: