Na Mwandishi Wetu.
Jeshi la Polisi Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya limefanikiwa kumkamata Raia wa Ghana, EMMANUELLA ADOM akiwa na kilo 6 za Dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya shilingi milioni 270.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za KULEVYA Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), GODFREY NZOWA alisema kuwa raia huyo alikamatwa hapo jana majira ya saa kumi usiku, kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam akitokea Nairobi Kenya kuelekea Accra, Ghana.
NZOWA alisema kuwa mwanamke huyo alikutwa sakiwa na mabegi makubwa mawili na kila begi lilikutwa na kilo tatu za Dawa hizo.
Kamishina huyo alitaja baadhi ya maeneo nchini ambayo yamekuwa yakitumika zaidi kupitisha na kuingiza Dawa hizo kuwa ni pamoja na Bandari bubu zilizoko maeneo ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam na Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: