Maharusi,Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiaga watu mbalimbali waliofika ndani ya kanisa la Azania Front,mara baada ya kufunga ndoa takatifu, mapema leo mchana jijini Dar.
Maharusi wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa na kuwa mwili mmoja mapema leo ndani ya kanisa la Azania Front,jijini Dar.
Maharusi wakilishana kiapo cha ndoa mbele ya umati mkubwa (haupo pichani) uliofika kanisani hapo mapema leo mchana kuishuhudia ndoa hiyo ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi,iliyofanyika ndani ya kanisa la Azania Front.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa akizibariki pete za ndoa za maharusi kabla ya maharusi hao kuvishana.
Baadhi ya Wanakwaya kutoka mkoani Arusha wakiimba
Umati wa watu uliofika kuishuhudia ndoa ya Bw.Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi iliyofanyika mapema leo mchana ndani ya kanisa la Azania Front,jijini Dar.
Maharusi wakiingia ndani ya kanisa la Azania Front mapema leo mchana,tayari kwa kufunga ndoa takatifu,pichani shoto ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Mh Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakishuhudia pia tukio hilo adhimu na la kihistoria kwa Wanandoa.
Maharusi Bw. Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiwa na wapambe wao wakielekea kanisani, tayari kwa kufunga ndoa takatifu, mapema leo mchana. Picha na Michuzijr Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: