Bi. E. Mrema (katibu wa UTU msaafu akimuongoza Bi. Ndata kuelekea kwenye viwanja vya sherehe katikati yao kwa nyuma ni Neema Ndesamburo Mtanzania) Mama Esther Kabwai mmoja wa maafisa wa ubalozi akibadilishana mawazo na mwana UTU Bw. Gaston Francis.
Hongera mama kwa kumtunza baba, maneno yaliotoka kwa kina mama wakitanzania waishio Uganda wakati wakimkabidhi zawadi yake.
Mh. Ndata akifurahia zawadi yake baada ya kufunguliwa.
Bw. Maugo akionyesha zawadi nzuri ya saa aliyopewa na UTU kama shukurani kwa mchango wake.
Bi. Ndata akiwa pamoja na afisa utawala wa Ubalozi na mjumbe kamati kuu ya starehe UTU, Anisa Mbega wakifurahia chakula.
Mwenyekiti mpya wa UTU Bw. Alphonce Mabiki akiwa na mkewe Mama Josephine Mabiki wakipata chakula.
Watoto wa Mwenyekiti mpya wa UTU kuanzia kushoto Eliza, Vero na Judy Mabiki wakitafakari utamu wa chakula.
Bw. Wilhelmina Balyagati mwanakamati mstaafu wa UTU na corporate and public Relation Officer (IUCEA) akitoka kuchukua chakula.
Kushoto ni Bw. Peter Musaroche mkuu wa maburudisho Umoja wa Wanafunzi Wakitanzania Bugema University (BUTASA) akiwa pamoja na Bw. Venance Raisi mstaafu Umoja wa Wanafunzi wa Kitanzania Makerere University na Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanafunzi Wakitanzania nchini Uganda.(TANSTUDENT).
Bw. Mahugo aliekuwa mkurugenzi mtendaji KASOWA wakifurahi pamoja na Mh. Ndata.
Mwenyekiti mstaafu wa UTU Dr Benedict Mtasiwa (Programmes and projects Officer wa (IUCEA) akiwa na pamoja na Neema Ndesamburo mwana UTU na Mama Esther.
Mama Esther Kabwai mmoja wa maafisa wa ubalozi akibadilishana mawazo na mwana UTU Bw. Gaston Francis .
Muweka hazina (UTU) Bw. Reuben Tumbwene
Bw. Grace kijuu Blom M/kiti msaidizi UTU pamoja na Wanzira Wambura Makamu wa raisi Management Club Bugema University ktk sherehe hizo.
Kulia ni Bw. Gabriel Ndata (kitinda mimba cha mh.) akiwa na rafiki yake wa karibu.
Hii ni moja ya zawadi aliyozawadiwa Mh.kaimu Balozi kwa njia ya sanaa na vijana kutoka Bugema University Peter Musaroche na Isack Ochaka.
Mh. Ndata na mkewe wakisakata twisti.
Bw. Kilindu Afisa wa ubalozi na mkuu wa nidhamu na usalama (UTU) akiwa na mkewe wakionyesha utaalamu wakusakata Rumba.
---
Uongozi wa Umoja wa Watanzania Uganda(UTU) ikishirikiana na Ubalozi iliandaa sherehe za Muunganiko wa matukio matatu muhimu kama ilivyo ainishwa hapo juu katika viwanja vya ubalozi vilivyoko katika mtaa wa shimon barabara ya Kegera jijini Kampala na kuudhuriwa na watanzania waishio Uganda.
Hafla hii ilifanyika tarehe 5/5/2012, ilitanguliwa na uchaguzi wa viongozi wapya wa UTU (ulifanyika mchana) na baadae jioni hafla ilendelea ambapo wanachama wa UTU na ubalozi walishereheke sikukuu za muungano, Mei mosi na kuwaaga mheshimiwa Ndata Kaimu balozi wa Tanzania nchini Uganda na Bw. Mahugo mwanachama mwenye mchango na mapenzi makubwa sana na UTU.
UTU chini ya uongozi wa mwenyekiti mstaafu Dr Benedict Mtasiwa (Programmes and projects Officer wa (IUCEA ) kwa ushirikiano wa karibu na wa hali na mali na mlezi wa wachama aliyekuwa kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Bw. Ndata walifanya mengi yakukumbukwa na watanzania waishio Uganda.
Yote yaliyofanywa na viongozi hao ilitokana na ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi waandamizi na kamati zake na watanzania waishio Uganda kwa ujumla.
Mwenyekiti mpya mteule ni Bw. Alphonce Mabiki ambae amepokea gurudumu la muendelezo wa mafanikio ya umoja wa watanzania waishio Uganda.
Toa Maoni Yako:
0 comments: