Hivi ndivyo Costa hii ya Mgumba yenye namba za usajili T 478 AGZ ilivyobanwa na lori.
Lori lenye namba za usajili T 508 AGG Scania likiwa limeibana costa mali ya Mgumba katika mlima wa Changarawe mjini Mafinga.
---
Na Francis Godwin, Iringa
Watu watatu wamekufa wengine 10 kujeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea jana na juzi katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Katika ajali ya kwanza iliyotokea usiku wa kuamkia jana Pamela S.Mbise anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 ambaye ni mke wa mfanyakazi wa Sao Hill Mufindi na dereva Taxi mjini Mafinga Edward Mgina pia anakadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 na 31 wamekufa papo hapo baada ya gari aina ya RAV 4 ambayo walikuwa wakitumia kusafiriki kuacha njia na kutumbukia katika mto Ruaha eneo la Misitu ya Sao Hill wilayani Mufindi .
Mashuhuda wa tukio hilo waliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa watu hao walikuwa wakitokea mjini Mafinga kwenda Sao Hill na baada ya kufika eneo hilo gari lao lilitumbukia mtoni na kushindwa kujiokoa baada ya gari hilo kugeuka mataili juu kutokana na kina kirefu cha maji katika eneo hilo na hivyo gari hilo kuonekana baada ya kupita masaa takribani mawili toka walipo zama katika mto huo.
Wakati katika ajali ya pili Costa mali ya Mgumba yenye namba za usajili T 478 BGZ iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kuelekea mkoani Iringa ilipata ajali eneo la Changarawe nje kidogo na mji wa Mafinga kwa kubanwa na lori lenye namba T 508 AGG na kusababisha kifo cha abiria wake Zainab Mkwawa ambaye alifariki dunia muda mfupi baada ya kupokelewa katika Hospital hiyo ya wilaya ya Mufindi ,Hospital ya Mafinga.
Mashuhuda wa ajali hiyo Kevin Kalinga alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva la Lori ambaye alikuwa ameliruhusu gari lao kupita na ghafla alizuia na kuibana costa hiyo .
Kwani alisema kuwa dereva wa Costa hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Zacharia alijitahidi kunusuru maisha ya abiria zaidi ya 30 waliokuwepo katika Costa hiyo bila mafanikio baada ya dereva wa lori hilo kulibana gari hilo la abiria ambalo pia lilikuwa likipandisha mlima .
Mganga mfawidhi wa Hospital ya wilaya ya Mufindi Dkt Ugene Lutambi alithibitisha kupokea Hospitali hapo kwa matibabu .
Alisema kuwa majeruhi waliofikishwa Hospitali hapo kuwa ni wanawake 6 akiwemo Bi.Zainab Mkwawa ambaye alifariki na wanaume watano.
Dkt Lutambi aliwataja majeruhi hao kuwa ni Upendo Msambwa (29) na Petrol Msisi (28) ambao wote ni makondakta wa Costa hiyo ya Mgumba .
Wengine ni Maria Mpete(50), Jane Ngailo (30), Evline Christopha (34),Amil Nyalusi (20) Eloi Mbilinyi (40), Issac Ndane (16), Anjelina Chapuga na Costa Ngailo ambaye alikimbizwa katika hospital ya mkoa wa Iringa kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.
Dkt Lutambi alisema kuwa hali za majeruhi zaidi 6 zanaendea vema baada ya kutibiwa na kuruhusiwa na abiria wanne ndio bado wamelazwa huku majeruhi Petrol Msisi na bi Maria Mpete wanaendelea vema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: