Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Bianadamu (LHRC) Bi. Hellen Kijo Bisimba akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusiana na tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete.
Ndugu wanahabari na wananchi kwa ujumla,
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tumefuatilia kwa makini
sana mchakato
wa Katiba mpya kuanzia ulipoanza mpaka hapa ulipofikia. Sote tunafahamu kwamba
hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kuteuliwa na kuapishwa kwa wajumbe wa tume ya
kukusanya maoni juu ya mchakato mzima wa Katiba mpya na namna ambavyo wananchi
wangependa iwe.
Tunependa kupompongeza sana
Mheshimiwa Rais na Serikali kupitia wizara ya Katiba na Sheria kwa hatua
iliyofikiwa mpaka sasa kwenye mchakato mzima. Tunatoa pongezi kwa uteuzi
wajumbe wengi waliobobea katika fani mbalimbali za Sheria, Siasa na Masuala ya kijamii.
Tumefurahi kuona kuwa Mheshimiwa Rais amemteua
kuwa mwenyekiti wa Tume Jaji
Joseph Sinde Warioba ambae tulishaona kazi yake nzuri hususan pale alipoongoza
vizuri tume ya Rais iliyohusu masuala ya Rushwa. Tuna imani kuwa ataongoza tume
hii kufanya kazi nzuri. Wajumbe wa Tume
hii ni 32 (akiwemo mwenyekiti na
makamu) waliapishwa tarehe 13/04/2012.
Wajumbe hao ni kama
ifuatavyo;
Mwenyekiti wa Tume ambaye ni Jaji Sinde Warioba na Makamu
Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Agustino
Ramadhani.Wajumbe wa tume toka Tanzania Bara ni Prof. Mwesiga L. Baregu, Nd.
Riziki Shahari Mngwali, Dr. Edmund Adrian Sengodo Mvungi, Nd. Richard Shadrack
Lyimo, Nd. John J. Nkolo, Alhaj Said El- Maamry, Nd. Jesca Sydney Mkuchu, Prof.
Palamagamba J. Kabudi, Nd. Humphrey Polepole, Nd. Yahya Msulwa, Nd. Esther P.
Mkwizu, Nd. Maria Malingumu Kashonda, Mhe. Al-Shaymaa J. Kwegyir (Mb), Nd.
Mwantumu Jasmine Malale Na Nd. Joseph Butiku. 2 Wajumbe wengine 15 ni kutoka Tanzania Zanzibar. Wajumbe hao
ni Dkt. Salim Ahmed Salim, Nd. Fatma Said Ali, Nd. Omar Sheha Mussa, Mhe. Raya
Suleiman Hamad, Nd. Awadh Ali Said, Nd. Ussi Khamis Haji, Nd. Salma Maoulidi,
Nd. Nassor Khamis Mohammed, Nd. Simai Mohamed Said, Nd. Muhammed Yussuf
Mshamba, Nd. Kibibi Mwinyi Hassan, Nd. Suleiman Omar Ali, Nd. Salama Kombo
Ahmed, Nd. Abubakar Mohammed Ali na Nd. Ally Abdullah Ally Saleh.
Mapungufu tunayoyaona;
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tunaona mapungufu
makubwa mawili kwa tume hii
i) Kuwemo kwa mbunge na mjumbe wa baraza la wawakilishi
ii) Uwakilishi finyu wa kijinsia na makundi mengine mfano
vijana
Wawakilishi kuwa wajumbe
Kituo hakikubaliani kabisa na uteuzi wa wakilishi wa
wananchi (Mbunge na Mjumbe wa Baraza la wawakilishi). Wajumbe hawa ni Mhe.
Al-Shaymaa J. Kwegyir (Mb) Tanzania Bara na Raya Suleiman Hamada mwakilishi
Baraza la Wawakilishi Zanzibar .
Sababu kubwa za kutokukubaliana na uteuzi wa wajumbe hawa ni
kuwa kwanza,
hawa watashiriki kama
wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba (constituent assembly) kwa hiyo kuna ‘mgongano
ulio dhahiri wa kimaslahi’. (kwa mujibu wa vifungu cha 6 na 22 (1) (a) na (b)
vya sheria Namba 8 ya Mabadiliko ya Katiba, 2011)
Pili wananchi wanaowawakilisha watanyimwa haki yao ya kuwakilishwa kwa kipindi
chote cha miezi 18 mpaka ishirini ambacho tume itafanya kazi kwa mujibu wa
sheria.
Tatu, kuna majina mengi ambayo mheshimiwa Rais alipelekewa
yenye sifa za kutosha angeweza kuwateua. Kulimbikiza kazi nyingi kwa watu wale
wale si afya kwa demokrasia.
Uwakilishi finyu wa kijinsia na makundi mengine
Katika tume hii tumeona kuna uwakilishi finyu sana wa makundi kwa mfano
wanawake wako 10 kati ya 32, yaani sawa na asilimia 27% tu! Tungetegemea asilimia
50% kwa 50% kwani Tanzania
imesaini na kuridhia mkataba wa nyongeza wa maendeleo ya kijinsia kusini mwa
Afrika yaani SADC Gender Protocol. Pia 3 Tanzania ina asilimia ya 51 ya
idadi ya wanawake ambao miongoni mwao wengi wana utaalamu na sifa za kuteuliwa
kuwa wajumbe wa Tume.
WITO
I) Tunapenda kutoa wito kwa serikali kuwa mchakato wa Katiba
ni wa muhimu sana
hautakiwi kuchukuliwa kwa wepesi. Mchakato huu unajenga mustakabali wa
Taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Hivyo katika maamuzi yote yanayochukuliwa,
kuwe na jicho la HAKI ZA BINADAMU na utawala wa sheria.
II) Pia tunapenda kutoa wito kwa WANANCHI wote wa Tanzania ,
mijini na vijijini, wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara, TUSHIRIKI kwenye mchakato
huu. Tunawasihi kuwa Tume ya Katiba itakapokuja kwenye
maeneo yetu tuhudhurie mikutano yote na kutoa maoni yetu juu
ya Katiba Mpya. Wananchi katika makundi au mtu mmojamoja anaweza kupeleka maoni
ya maandishi kwenye tume mara anuani itakapojulishwa kwa wananchi.
III) Mwisho tunatoa wito kwa tume kuhakikisha watu wote
wanatoa maoni yao
bila ubaguzi. Makundi yote ya jamii yafikiwe (Wanawake, wanaume, watu wenye
ulemavu na watoto wenye umri wa kutoa maoni).
Asanteni kwa kunisikiliza,
Dr. Helen Kijo-Bisimba
Mkurugenzi mtendaji- LHRC
Toa Maoni Yako:
0 comments: