TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Blantyre , Malawi
leo jioni kuhushuria Mazishi ya Profesa Bingu wa Mutharika, aliyekuwa Rais wa Malawi, aliyefariki
tarehe 5 April, 2012 Kufuatia matatizo ya Moyo
Rais Kikwete ni miongoni mwa Viongozi wakuu Saba kutoka nchi
jirani na Malawi . Nchi hizo ni Afrika Kusini , Benin , Kenya ,
Msumbiji , Zimbabwe
na Zambia .
Wakati huohuo Ikulu inapenda kukanusha taarifa
zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari
kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya
hatua za kuwachukulia Mawaziri
wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika Wizara zao.
Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.
Pia nitumie nafasi hii kuwatahadharisha waandishi wa habari
kuwa makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na kuandika au kutangaza
taarifa wanazopata.
Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa
Ziara ya kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.
Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa
Waziri Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la tuhuma hizo limetokea
Bungeni.
Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu,
basi atakua amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua hatua inayofuatia.
Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari
kueneza uongo na fitna zenye lengo la
kuchonganisha si viongozi tu , bali hata viongozi na
wananchi kwa ujumla.
Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho tarehe 23 April
mara baada ya maziko.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
22 April, 2012
Toa Maoni Yako:
0 comments: