MSANII Nassib Abdul ‘Diamond’ ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya kujinyakulia tuzo tatu. “Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond mara baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.  Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes. Barnaba aliibuka Mwimbaji Bora wa Kiume, akiwashinda, Ally Kiba, Diamond, Belle 9 na Mzee Yussuph.
MSANII Nassib Abdul ‘Diamond’ akiwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura.
Ommy Dimpoz na Diamond pamoja na mama yao mara baada ya kupata tuzo.

Muigizaji/mchekeshaji Mahiri wa kikundi cha Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku akimkabidhi tuzo yake msanii Diamond, ya video bora ya mwaka.

kaka
Mume wa mwanamuziki Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee, Bw. Gadna G. Habash akiwapokea tuzo kwa niaba ya mkewe mara baada ya kupata tuzo tuzo ya Msanii bora wa Kike.

Msanii Mahiri kutoka THT,Barnaba akipokea tuzo ya Msanii bora wa kiume kutoka kwa mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu.
Prodyuza Maneka wa AM Records akikabidhiwa tuzo yake ya Prodyuza bora wa muziki 2012.


H.Baba akiwa na mchumba wake.
Mwanamuziki mkongwe wa taarabu nchini,Bi Shakila akiwa na tuzo ya waliochangia mafanikio ya muda mrefu ambayo pia ilikwenda kwa JKT Taarab.
B-12 na Dj Fetty.

Hata sisi tulikuwepo.



Dogo akiwa amekoleza mduara.
Mwanadada Shilole nae aliweza kuburudisha vilivyo.
Vijana wakifurahia kwa pamoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: