Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Mh Zitto Kabwe ametaarifu katika mtandao wa Jamii (Twitter) kuwa mpaka sasa zimeshakamilika kura 62 za Wabunge ili zikamilike70 ili kuweza kupeleka hoja ya kulitaka Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Zitto amesema kuwa zoezi zima la saini hizo limeanza asubuhi wakati wakiingia Mlangoni ili kabla ya Jumatatu liwe limekamilika ili kuweza kuwasilisha hoja hiyo ili Wabunge na Bunge limshinikize Waziri Mkuu kujiuzulu au vinginevyo mawaziri wote waliotajwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wawe wamejiuzulu badala yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: