Shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu, Wazazi wangu, Family yangu, Mh; Joseph Mbilinyi (Sugu), Ghetto BoyZ, Watupori, Producers, wadau wa media zote, wana morogoro, fans wangu, na artist (musician) wote wa Afrika Mashariki. katika miaka 36 (24-4-1976- 2012), wameniwezesha kutimiza ndoto yangu ya kutumia kipaji changu katika kuelimisha jamii, siku zote naamini katika haya maneno "Fungua kinywa chako kwa ajili ya mtu asiyeweza kusema, ili kutetea watu wote wanaopitilia mbali, Fungua kinywa chako kutetea mtu mwenye kuteseka na umasikini"

Kupitia hayo/wao nimeweza kuwa na Album Nne Ambazo ni MKUKI MOYONI, DARUBINI KALI, NAFSI YA MTU na HESHIMA, album ya tano KINGDOM wakati wowote kuanzia sasa itakua sokoni, na Kuwa KING OF RHYEMES IN TANZANIA (BONGO) HIPHOP/FLAVOUR.

Kama tunasheherekea siku ya kuzaliwa, basi tukumbuke kuna siku ya kufa vilevile, siku ya kuzaliwa iwe changamoto kwetu sote kwa kutathimini sababu za uwepo wetu duniani, na kusudi la muumba kutuumba wanadamu, na si wanyama, ndege, wadudu au samaki.

Lakini pia tujifunze kuwa maisha (kuishi) ndio zawadi kubwa na ya pekee aliyotupa Muumba wetu. Tuyatunze maisha yetu na ya wengine kwa kutenda Haki bila kikomo, na kusameheana, hakuna alie mkamilifu. MUNGU AWABARIKI.

Asanteni.

SELEMANI ABDALLAH JUMA MUTABHAZI MSINDI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: