Rais Jakaya Kikwete leo amefunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa Mkoani Iringa. Pamoja na kuhutubia katika kilele hicho pia Rais alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya watoa huduma za maji na wadau mbalimbali wa maji nchini. Pichani ni Rais Kikwete akiwa katika banda la Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa maadhimisho hayo ya mwaka huu yaliyofanyika uwanja wa Samora Mjini Iringa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Meneja Uwajibikaji na Miradi Endelevu wa SBL, Nandi Mwiyombela.
 Rais Jakaya Kikwete akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na Kupokelewa na Mkurugenzi wake wa Mahusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda. Pia SBL walipokea Cheti cha ushiriki wa maonesho hayo.
 Meneja Uwajibikaji na Miradi Endelevu wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Nandi  Mwiyombela,akisaliamiana na kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete katika banda la Kampuni ya Bia ya  Serengeti lililopo katika viwanja vya Samora mjini Iringa yalipofanyika maonesho ya wiki ya Maji kitaifa. Zaidi na zaidi gonga hapa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: