TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

UTANGULIZI

Baada ya kikao cha madaktari kilichofanyika leo tarehe 10/3/2012. Madaktari nchini kupitia chama cha madaktari Tanzania (MAT), tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

1. Jamii ielewe kuwa daktari kama binadamu mwingine anayefanya kazi Tanzania ana mahitaji muhimu (basic needs) na mahitaji ya kijamii (social responsibility) na hivyo si chombo cha kufanyia kazi (Machine).

2. Pia Daktari ana haki ya kupata ujira unaomfaa kutokana na kazi anayofanya na ana haki ya kuacha kazi muda wowote iwapo ataona kazi hiyo ya udaktari haimpi ujira wa kutosha na heshima ya kuendesha maisha yake.

3. Pia jamii itambue kuwa daktari anaweza kulazimishwa kurudi kazini lakini hawezi kulazimishwa kufanya kazi. Matokeo ya kulazimishwa yanaweza yasiwe mazuri kwa wale watakao hudumiwa.

4. Jamii itambue kuwa madai na hoja kuu za madaktari ni kwa ajili ya faida ya Watanzania wote,yakiwemo mazingira bora ya kufanya kazi mjini na vijijini, na kuboresha afya za watanzania kwa ujumla. Pia vifaa na dawa ziwepo mahospitalini zinakohitajika.

5. Pia tunawashukuru madaktari wote kwa mshikamano wetu tulioonyesha na tunaomba mshikamano huu uendelee daima.

TAMKO LETU:

JANA TAREHE 9/3/2012, TULIKUTANA NA MH. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE. TULIMWELEZA HOJA ZETU, AMBAZO ALIZIELEWA NA ALIAHIDI KUZISHUGHULIKIA KIKAMILIFU. TUNA IMANI SANA NA MH. RAIS KWAMBA HATATUANGUSHA.

KUTOKANA NA HILO, TUNAPENDA KUUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KUWA TUNARUDI KAZINI RASMI KUANZIA LEO TAREHE 10/3/2012, WAKATI MHESHIMIWA RAIS AKISHUGHULIKIA MADAI YETU.

PIA WAKATI MADAI YETU YAKISHUGHUKLIKIWA TUNAPENDA KUSEMA KUWA HATUNA IMANI NA WAZIRI WA AFYA MH. DR. HAJI MPONDA NA MH. DR. LUCY NKYA, NA KUWA TUNAMSIMAMISHA RASMI UANACHAMA WA MAT MH. DR. LUCY NKYA.

MADAKTARI TUNATAMKA WAZI KUWA WAZIRI WA AFYA DR. HAJI MPONDA NA NAIBU WAKE DR. LUCY NKYA NI MAADUI WA MADAKTARI NA SEKTA YA AFYA KWA UJUMLA HAPA NCHINI NA TUNAAHIDI KUTOKUWAPA USHIRIKIANAO WA AINA YOYOTE WA KIBINAFSI AU WA KIUTENDAJI.

SOLIDARITY FOREVER.

KATIBU MKUU - MAT
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: