Na Gladness Mallya, Global Publisher
KWA mara ya kwanza msanii wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ (pichani) amefunguka: “Kiukweli sanaa inatufanya wasanii wa kike tuingie kwenye vitendo vya umalaya.”
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Koleta alisema, kutokana na sanaa kuwa ngumu imesababisha baadhi ya wasanii wa kike wajihusishe na tabia hiyo mbaya.
“Sanaa ya Bongo ni vigumu sana kutoka, hailipi kabisa... yaani inatakiwa mtu ufanye kazi nyingine tofauti ndiyo uweze kufanikiwa. Wasanii unaowaona wamefanikiwa si kwa filamu pekee, wana mambo mengine,” alisema na kuongeza:
“Kwa bahati mbaya kuna wanaotaka kutumia njia ya mkato, hao wanajikuta wameangukia kwenye umalaya. Kwa sababu wanafanya mambo yao na jamii inawaona, wasanii wote wa kike tunahesabiwa ni malaya tu.”
Toa Maoni Yako:
0 comments: