Kanuni ya Kwanza….
Huruhusiwi kumuoa Mwanamke mpaka akuletee CV yake ili ukague kama shuleni alishiriki Michezo ya kurusha Tufe na Ndondi. Hii itakusaidia kumchagua mtu right!
Pili, Mwanamke anapoanza kukudunda unaruhusiwa kutuma please Call me kwenye 911 ya Police!
Tatu, Mwanamke haruhusiwi kumpiga Mwanaume akiwa Soba, ni lazima Mwanaume awe amelewa ndo umdunde ili kuepusha Maumivu ya dhati.
Nne, Kwa kuwa wanaume wanaopigwa na wake zao huwa wanadanganya Ofisini kwamba wameanguka au wamekabwa na vibaka, tumegundua huo uongo umepitwa na wakati kwa hiyo Chama kimeamua kuwaajiri waandishi wa script za Filamu za Kibongo ili wasaidie kuandaa Uongo mpya!
Tano, Kanuni nyingine ni kwamba kila Mwanaume unapopigwa, nenda ukweni upunguze kitu kimoja kwenye Mahari uliyotoa. Kama ulitoa Mahari ya Ng’ombe 10 baada ya Vipigo tisa tunategemea kitakuwa kimebaki kipigo kimoja tu umalizie Ng’ombe wako wa kumi na ndoa kwisha!
Sita, Marufuku kwa Mwanamke kumpiga mme wake kwenye Foleni unless gari liwe na vioo vya Giza, tinted! Lakini ikitokea ulazima, Mwanaume ukipigwa kwenye gari lisilo na tinted jifanye unacheza ile style ya Busta Rhymes katika wimbo wa Arab Monay!
Saba, Kwa wakati huu ambapo kuna mgao wa umeme, kwa hivyo redio na TV zinakuwa zimezimwa, ni marufuku kwa Mwanamke kumpiga Mmewe kwa kuwa Sauti zitaenda mbali.
Nane, Mwanaume unapopigwa ni lazima kulia kwa kutaja jina la Chama na sio ulie Mamaaa!
Tisa, Mwanamke unatakiwa unapompiga mmeo iwe ni mwisho wa mwezi au tarehe kama hizia ili jioni asirudi na awe na pesa ya kusogeza katika mbili tatu baa ya jirani.
Na Kanuni ya Mwisho ni lazima siku ambayo mama umepanga kumpa Kipigo Baba, watoto wote wawe wamepelekwa kwa Bibi kwa kisingizio cha kwenda kusimuliwa hadithi za kale!
Hizo ni Kanuni 10 za Katiba ambayo bado ni Rasimu na una nafasi ya kuongeza Kanuni nyingine kupitia namba 0786 000884 na utajibiwa na Mwenyekiti Paulo James au Katibu Gerald Hando! Barbara ni shahidi tu! Ova!
Imeandaliwa na Detective, Chairman wa CCWWT - PJ na Katibu Gerald Hando kwa niaba ya wanachama wote wa CCWWT.
Toa Maoni Yako:
0 comments: