Wakazi wa jiji la Mwanza leo wamelazimika kutembea kwa miguu mara baada
ya madereva wa mabasi madogo maarufu kwa jina la daladala kugoma
wakishinikiza dreva mwenzao aliyewekwa lockup' aachiwe huru, kwani
imekuwa kawaida sasa kwa wasimamizi hao wa usalama barabarani
(matrafiki) kuwanyanyasa madreva na makonda kwa kuwabandikia makosa. Madereva hao wamelalamikia ushuru wa zaidi ya shilingi 6,500/= kwa siku
yaani tozo la shilingi 500/= kwa kwenda na kurudi 500/= sawasawa na
shilingi 1,000/= kila safari, badala ya shilingi 500/= kwa siku kama
inavyofanyika mikoa mingine. Dereva aliyeswekwa lockup' tangu jana bwana Protas B Son, baada ya kosa kubwa ameachiwa kinyemela bila dhamana leo alfajiri mara baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kuwa kuna mgomo umeandaliwa kufanyika kuanzia leo.
Pia Bodaboda pamoja na pick up leo zimekuwa siku kuu kwao...
Pichani wakazi wa jiji la Mwanza wakiwa wamepanda gari la mizigo maarufu kama 'pick up' ikiwa imebeba abiria kuelekea mjini.
Mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala kanda ya ziwa Protas Dede amewaomba radhi wananchi kwa hali iliyotokeza na usumbufu walioupata kwani imewabidi kutetea haki ili mambo yaende sawa.
Wamiliki wa Dalada wakiwa wamepaki vyombo vyao vya usafiri mbele ya ofisi za wilaya uwanja wa Ghand Hall kusubiri mkutano na RTO.
Habari/Picha: gsengo blog
Habari/Picha: gsengo blog
Toa Maoni Yako:
0 comments: