Ujumbe kutoka kwa wanaharakati hao.
Ujumbe wa kuishinikiza serikali iweze kukaa chini na madaktari ili wajadili.
Mkurugenzi wa TAMWA,Mama Ananilea Nkya (kulia) akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mbalimbali kuhusiana na maandamano yao yaliyodumu kwa muda wa masaa mawili hivi kwa ajili ya kuishinikiza Serikali ikae meza moja na madaktari na kuhakikisha mgomo wao unakoma mara moja na kuhakikisha shughuli za matibabu hospitali ya Muhimbili na nyinginezo zinaendelea kama kawaida.
Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Bi Hellen Kijo-Bisimba akiwa ameshikilia nango lenye ujumbe kwa serikali ukimtaka rais Jakaya Kikwete kuwafuta kazi mara moja Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr Haji Mponda, Naibu waziri wake Dr Lucy Nkya, Katibu mkuu Blandina Nyoni na Mganga mkuu Dr Deo Mutasiwa kwa kushindwa kuzuia mgomo wa madaktari nchini. Aliyekaa katikati ni mkurugenzi wa Tamwa Ananilea Nkya na kushoto ni Anastazia Rugaba wa HakiElimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: