Ulimwengu uliotawaliwa na mitandao ya kijamii, ni ule unao wasaidia wafanyabiashara kufikia malengo yao. Tigo kwa kulitambua hilo ikafungua ukurasa katika mtandao wa facebook,na kujikuta kwa kipindi kifupi inaibuka kuwa na mashabiki wengi wanaotembelea ukurasa huo kuliko kurasa za makampuni mengine ya simu nchini.
Ukurasa wa Tigo katika face book unatoa habari mbalimbali kuhusu Tigo pamoja na huduma zake, ni sehemu inayowaunganisha mashabiki wa Tigo na kuwawezesha kuchangia mambo na kampeni mbalimbali zinazoanzishwa na Tigo,vilevile mashabiki wanapata fursa ya kujua huduma na bidhaa mpya zinazotolewa na Tigo
“kuhakikisha tunakuwa karibu na wateja wetu katika ukurasa wetu wa face book tunahakikisha wateja wetu wanaendelea kuridhika na huduma zetu” anaelezea Mr. Gonzaga Rugambwa msimamizi wa ukurasa wa Tigo katika face book anaongeza kuwa “face book inatoa nafasi ya kubadilishana mawazo na ndiyo maana tumechagua kuutumia mtandao huu wa kijamii”
Mr. Rugambwa anaendelea kwa kusema kwamba Tigo ina furaha sana kuwa moja ya kampuni inayopendwa sana nchini Tanzania hasa kwenye mitandao ya kijamii,na ana waomba mashabiki wake kuendelea kuwapa ushirikiano na anasisitiza kuwa kujitolea kwao katika ukurasa wa Tigo facebook ndio unaosababisha ukurasa huo kuwa mahali pazuri pa kupata taarifa na kujadiliana.
Kwa kujiunga na ukurasa huo mashabiki wanapata nafasi ya kupewa taarifa za mambo muhimu yanayoendelea, pia mashabiki wana uwezo wa kuwaalika marafiki na jamaa zao kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa ‘share’ pia kwa kutumia upande wa kushoto katika ukurasa wa Tigo mashabiki wanaweza kuangalia video kutoka ‘you tube’,kutembelea mtandao wa ‘ tweeter’ na kupata huduma kwa mteja kwa saa ishirini na nne,ambapo wanaweza kutuma malalamiko na mapendekezo yao na kujibiwa katika muda muafaka.
Ukurasa wa Tigo facebook ni sehemu nzuri ambayo wateja wa Tigo wanapata huduma kwa mteja ya hali ya juu pia ukurasa wa Tigo face book unawapa fursa wateja kutoa dukuduku zao kwa mtandao wao wanaoupenda wa Tigo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: