ACP Kashai akikagua kikosi cha kupambana na majambazi kwa kutumia piki piki.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai akikagua kikosi cha kutuliza ghasia na mafunzo aliyotoa kukabiriana na majanga.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai, akikagua kikosi cha makachelo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai akifundisha.
---
Na Pardon Mbwate Mwandishi wa Jeshi la Polisi- Kigoma
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai, alitoa wito kwa kila Askari Polisi mkoani humo kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa kuzingatia taratibu na sheria na kudumisha huduma bora kwa mteja.ili kuepuka malalamiko dhidi ya Polisi.
Kamanda Kashai alitoa wito huo wakati akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali katika mkutano uliofanyika leo kwenye Viwanja vya FFU mjini Kigoma.
Alisema dhamira ya Jeshi la Polisi ni kuona kuwa kila mwananchi anayefika katika kituo chochote cha Polisi anapata huduma bora kama anavyotarajia.
Kamanda Kashai ambaye awali alikagua gwaride lilikoandaliwa na Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasi na makachero mkoani humo, amesema jukumu la kila askari ni kuona kuwa kila mmoja anafanya kazi kwa kujituma na kwamba kwa upande wake Kamanda huyo amesema ataendelea kutoa elimu kwa askari juu ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi.
Alisema kutokana na mabadiliko ya mifumo ya Majeshi ya Polisi Duniani, Polisi anatakiwa kumuona Raia kuwa ni sehemu ya Polisi na Raia naye amuone Polisi kama ni sehemu ya Raia ili kujenga kuaminiana.
Alisema kuwa utendaji wa Jeshi la Polisi unategemea sana taarifa za wananchi katika kuwafichua wahalifu na hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa tunadumisha ushirikiano na kujenga ubia wa kweli baina ya Polisi na Raia wa Kawaida.
Kamanda Kashai pia alisema hivi sasa Jeshi la Polisi limelenga kusogeza huduma kwa wananchi zaidi ili matatizo yanapotokea yaweze kutatuliwa kwa haraka hata kabla ya kufika katika vituo vya Polisi.
Alisema ili kuboresha utaratibu huo, juhudi zimefanyika ili kuhakikisha kuwa kila tarafa na Kata wanapatikana askari wakuweza kushirikiana na wananchi punde linapotokea tatizo la uhalifu.
Tayari Kamanda Kashai alishaanza utaratibu wa kutoa elimu ya Polisi Jamii katika vituo vya Polisi mkoani humo ambapo Wakuu wa Vituo vya Polisi 18 na Askari 132 wa Vyumba vya Mashtaka katika vituo hivyo watanufaika na elimu hiyo nao kuisambaza kwa wenzao wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments: