"Nilimua kuimba mziki nikiwa FORM 2, nikaanza kwa kuubadilisha wimbo wa KAMANDA wa DAZ NUNDAZ na kuweka mashairi ya kuwaagia wenzangu kama ningefeli form 2, bahati nzuri nikafaulu hivyo nikamua kuanzisha kundi lililoitwa TATU KALI ndani yake akiwemo CHARLES NA LEORNARD tukawa tunafanya poa kwenye matamasha ya skuli japo shule ilikuwa kijijini mbaya huko MANYARA - BABATI - KIJIJI CHA MJERUMANI... hatukuweza kurecord mpaka namaliza form four... nikasimama kidogo mziki but nilivyoingia kidato cha tano pale BISHOP DURNING HIGH SCHOOL… nikaamua kurudi tena kwenye mziki safari hii nikiwa mwenyewe nikijiita MWANAJESHI WA MKWAWA, nakumbuka nilikuwa na mshkaji wangu PIUS KIMATI au DAZ kutoka kundi moja lilikuwa hapo hapo skuli linaitwa WAKAGUZI...
Siku moja nikashiriki kwenye shindano la kuimba lililokutanisha shule kumi lilikuwa shindano la ISHI KAMPENI, mimi na mwanangu DAZ tukashinda nafasi ya pili na kupewa shilingi elfu 60,000/= basi nikaupenda sana mziki kiukweli na nakumbuka nilimpenda dada mmoja hivi anaitwa ROSE akaniletea pozi sana nikamtungia wimbo mmoja unaitwa LOVER T nikauimba kwenye show moja skuli yule girl akanikubali na nikawa mpenzi wake.. Nikawa famous sana skuli... so yakawa maisha yangu mimi na muziki na skuli...
  
Nakumbuka nilipomaliza kidato cha sita nikafanya show ya mwisho kwenye GRADURATION nikiwa na mshkaji wangu PIUS KIMATHI na kwa mara ya kwanza nikapiga picha ya karibu nikiwa nimevaa suti kali sana.. sasa ile pic nikaichukua na kuipeleka HOME nikampa baba akaiwekea kwenye frame na kuitundika sebuleni. Hapo ukawa mwisho wa mimi kuonana na wale nilikuwa nawajua kuwa wanafanya mziki pale skuli na mpaka hapo sikuwa nimerecord wimbo wowote.... Siku moja nikawa naitazama sana ile picha ambayo imewekwa sebuleni nikajiuliza HIVI SI NDIO WANAVYOVAA WATANGAZAJI WA TAARIFA YA HABARI?? SO HATA MI SINAFAA PIA?? hilo wazo likanizunguka sana kichwani huku mara kwa mara nikiijaribu sauti yangu kama inafaa kutoka kwenye kuimba kwenda kwenye kutangaza... nikaikumbuka kauli ya mama yangu ambaye baada ya kuwa namsumbua sana nikiwa mdogo aninunulie TAPE za wanamuziki wa kurap akanambia "WEWE UTAKUJA KUWA MTANGAZAJI WEWE MAANA UNAPENDA KWELI KUWAFAGILIA NA KUWAONGELEA WANAMUZIKI WA KUFOKAFOKAA" nikaamua kumwambia baba kuwa nahitaji kusoma utangazaji. 

Baba hakukataa nikaianza safari yangu ya kuja na Dar na kusoma utangazaji huku nikiwa nimedhamiria kuwa ni lazima ndoto yangu itatimia tu" NIMEAMUA KUHADITHIA HII ITAKUSAIDIA KWA NAMNA FULANI WEWE KAMA RAFIKI YANGU… Basi nikafika mpaka DSM na kuanza kusoma journalism pale DSJ ILALA, nikiwa naishi hostel maeneo hayo hayo. siku ya kwanza tu kuanza chuo nilijiskia vibaya sana maana baadhi ya watu walinicheka na kunishangaa kisa lafudhi yangu ya ki-A TOWN, nikaona dah… ina maana hii lafudhi inaweza kunifanya mimi nisiwe mtangazaji kweli??? ila nikajiuliza kwani ADAM MCHOMVU na B12 wametokea wapi?? si ARUSHA?? hivyo nikawa napenda sana kumsikiliza GADNER G HABASH nikasema noooo! lazima niweze tu. 

Nikaamua kuwa kimya sana kwa wiki nzima ili nisichekwe.. lakini masomo yalivyoanza nikapata rafiki ambaye ni BARNABAS SHIJA, akanipa moyo na ndipo nikahamishia hasira zangu kwenye kitabu nikiwa na kampani kubwa ya watu kama kina SALAMA SALEHE, DENNIS DIDAS, FADHILI HAULE (Hivi sasa ni mtangazaji wa Capital radio), NOAH LALTAIKA (yuko EATV), YULIA MWAMBA na wengineo kibaooo... nakumbuka tulifanyiwa sherehe ya kukaribishwa chuo ambayo ilifanyika pale BAGAMOYO... nikajikuta nimetamani mic na kuimba kidogo siku hiyo baadhi ya watu wakaniambia plzzzz karecord bana laini akili yangu ikakataa na hapo ndio nikauacha mziki na kuamua kukaa upande wa utangazaji. kiukweli nilikuwa napenda sana somo la radio kuliko masomo mengine japo yote nilikuwa nafanya vizuri. 

Nawashukuru walimu wote wa DSJ hasa Mr. Rupepo (Mkuu wa chuo na my Brother pia), MWL. Edwin, MWL. Kimota na wengine wote. Nakumbuka mara yangu ya kwanza kabisa kutangaza nilikwenda FIELD PALE TANGA kwenye radio moja inayoitwa MWAMBAO FM... ambapo nilikuwa nachambua magazeti asubuhi na mchana pia nikawa nina segment kipindi cha mchana, nikatangaza mpaka kipindi cha malavidavi usiku. Nilifanya filed katika radio ile nikiwa nakaa gesti moja sikumbuki vizuri iko sehemu gani pale tanga kwa siku 45 kwa malipo ya 3000 kwa siku. baada ya hapo nikarudi chuo baada ya field ya pili nikaja kwenda MTWARA radio moja inaitwa PRIDE FM nikafanya field huku nikiwa naishi kwa washkaji zangu MOHAMED NA DJ STREETWISE... 

Pale nikawa natangaza kipindi kimoja kinaitwa MORNING CRUZ na dada mmoja anaitwa MARRY... Nikawa nimeshaizoea radio freeeesh kabisa. nikapongezwa sana na Mkurugenzi wa radio ile Mr. Rama.. akaniambia nikimaliza tu Chuo niende nikaanze kazi tukakubaliana basi nikawa na uhakika wa kazi sema mmmhhh! nikawaza sana kuishi Mtwara. Basi field ilivyokwisha nikageuza kurudi chuo. Nakumbuka wakati niko chuo kuna sherehe zilikuwa zikifanyika za kuwakaribisha wanafunzi wapya kila muhula mpya, sasa kwenye hizo sherehe nikajikuta nakuwa MC muendesha shughuli... nakumbuka sherehe moja ilifanyika pale WATER WORLD Mbezi na mgeni rasmi akawa BOSS RUGE.. na mimi nilikuwa MC.. akapenda sauti na mtazamo wangu kisha akaniambia nije Clouds nikasema ASANTE MOLA NDOTO IMETIMIA... sijui kiliningia nini kichwani nilipomaliza tu chuo nikaenda zangu MTWARA na kuanza kazi PRIDE FM Radio kama mtangazaji wa kipindi kile kile cha MORNING CRUZ.. ila lafudhi yangu ya kiA-TOWN ikawa imepotea kidogo... Nakumbuka siku hiyo niliingia NEWS ROOM nikaona karatasi za taarifa ya habari mezani nikaomba jamani naombeni nisome news leo.. daaaaaahhh watu wakabishana balaa hapana bwana huyu jamaa ana maneno ya kihuni atachanganya mambo kwenye usomaji... nikawaambia nipeni msiogope... nikapewa nikazama studio kumi kamili nikasoma news kwa mara ya kwanza.... kumbe mkurugenzi alikuwa anasikiliza akasema please Casto awe anasoma news na ghafla nikapewa cheo kamili kama PRESENTER & NEWS EDITOR.... Maisha yakaanza nikiwa na kagodoro kangu....

Nilipata wakati mgumu kidogo kutokana na maisha mapya niliyaanza MTWARA nikawa busy from monday to sunday.. maana nikawa natangaza mpaka top 20 jumapili saa nne mpaka saa sita.. ndani ya mwezi mmoja nikawa nimezoea kidogo. katika vitu ambavyo sitosahau nikiwa Pride fm radio nakumbuka kwa bahati mbaya niliwahi kutamka tusi nikiwa ON-AIR usiku kile kitu kiliniuma sana nikaona nimeidhalilisha taaluma yangu na ndipo nikajifunza kwamba ni dhambi na ni hatari sana kuingia studio kutangaza kipindi huku kichwani ukiwa na STRESS/MAWAZO AU UMETUMIA KILEVI CHOCHOTE KILE.

Mengi yalitokea ikiwemo mimi kung'ang'ania kucheza mechi kati ya RADIO YETU NA WANAKIJIJI nikakataliwa kisa sikuwa nikionekana kwenye mazoezi, lakini kwa kulazimisha nikacheza na nikafunga goli pekee la ushindi kisha nikavua jezi na kutoka uwanjani hahaa.... nalikumbuka disco moja la Mtwara pale kwenye ukumbi wa bandari maana kwa wakati ule ilikuwa ndilo maisha club ya kule. Kikweli kutokana na uongozi wa radio ile kutoeleweka katika makubaliano yetu ya mwanzo na kuanza kwenda kinyume nilianza kufikiria uamuzi wa kuacha kazi nikiwa nimefanya kazi kwa muda wa miezi miwili tu. 
Nakumbuka nilipigiwa simu na RAIS WA CHUO nilichosoma kwa wakati huo BW. SIMON SIMALENGA kwamba kama utaweza kuja Dar ningependa uwe MC wa suprise kwenye sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya nikamwambia nitacheki kama nitaweza. Nakumbuka ilikuwa siku ya alhamis nikiwa nimeshalipwa mshahara wangu wa mwezi wa pili kazini tena mshahara ambao haukuwa tuliokubaliana, nikaaga kwa uongozi ambao ulikuwa umenipa ahadi nyingi ambazo hazikuwa zikitimia kila siku. 

Nikatua mjini Dar nakurudi kwenye ile ile hostel ambayo nilikuwa nikikaa mwanzo ambayo nakumbuka kabla sijamaliza chuo jamaa mwenye hostel alinipa ofa ya kukaa bure na mimi nikiwa ndio boss ninayekusanya hela za wengine maana nampelekea Mkubwa FADHILI sitomsahau. Basi jumamosi nikampigia simu BW. Simon Simalenga nikamwambia niko Dar hivyo nitaweza kuwa MC kwenye ile sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi iliyofanyika palepale WATER WORLD tena basi akaniambia niende, nashukuru Mungu wanafunzi walifurahi sana kuniona na nikawa MC pale. Mungu si Athumani kumbe Bosi Ruge alikuwa ametuma watu wawili ambao ni (WASIWASI MWABULAMBO NA STELA) wakaniita katikati ya sherehe na kuniambia wanatafuta watu watakaokuwa watangazaji kwenye CLOUDS TV. Nikasema sawa mimi niko tayari wakaniambia niende ofisini Clouds siku ya jumatatu kwa ajili ya Screen Test nikaenda nikafanya na hatimaye nikaambiwa kwamba natakiwa kuja kuanza kazi Cloud Tv kama mtangazaji wa TV. 

Nikaanza kazi na nimefundishwa na nimejifunza mengi sana na naendelea kujifunza mengi sana nikiwa hapa Clouds. unaweza ukajiuliza heeeee!! sasa mbona ulikuwa unapenda radio na umekubali kuwa TV??? ukweli ni kwamba ukishaamua kuwa mtangazaji, kuwa tayari kwa TV au radio maana ni kazi moja sema tofauti yake ni kusikika na kuonekana. Kiukweli sitowasahau watu ambao walinisaidia sana katika kipindi cha kati nilichoishi Dar wakati nimeacha kazi Mtwara kama Mr. Ruge, Mr. Rupepo, Mr. Fadhili, Mr. Simon Simalenga, Mr. Wasiwasi pamoja na Sister Stela na Joyce Jonathan. Special thanks to My Father DICKSON LAMSON na My lovely Late Mother IMELDA EVAREST nyinyi ni nguzo kwangu. 

Hapa nilipo bado naamini sijafikia hata robo ya safari yangu bado nina mengi ya kukabiliana nayo lakini nimshukuru Mungu kwa nilipo na nimuombe anisaidie niendako. naahidi mengi mengi mazuri kwa wewe rafiki ambaye unanitazama kila siku kwenye my show ya SIZ KITAA ya CLOUDS TV kila siku saa moja na robo jioni. Marafiki zangu wote wa FACEBOOK na wasio FB, BBM, wafanyakazi wenzangu wote wa CLOUDS MEDIA GROUP na wa radio na TV zingine pia, waandishi wa magazeti, magazine, wana Blog wote bila kuwasahau maboss wangu asanteni sana MUNGU AWABARIKI DAIMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI OFISI YANGU CLOUDS MEDIA GROUP.

(ASANTE KAMA UMEJIFUNZA KITU KUTOKA KWENYE STORY YANGU YA KWELI.)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

4 comments:

  1. Dogo thats extremely inspiring, ujue mtu akikucheki first time anajua ndio wale wale fridge open, kumbe umeanzia mbali...na utafika mbali sana upon Gods grace, a very big up to you mwananchi wa kawaida. Inspiry

    ReplyDelete
  2. Big Up Kaka tupo pamoja.

    Ezra wa Kigogo Sambusa

    ReplyDelete
  3. Moja ya watangazaji ambao nawakubali sana ni wewe. Kaza buti

    ReplyDelete
  4. Moja ya watangazaji ambao nawakubali sana ni wewe. Kaza buti

    ReplyDelete