Naibu waziri wa Tamiseni Agrrey Mwanri (kushoto) akimhoji mhandisi wa ujenzi wilaya ya Kilolo Atu Mwaipyana juu ya kiwango cha Elimu yake, katikati ni M bunge waJimbo la Kilolo Prof. Peter Msolla

IKIWA ni siku mbili baada ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Agrrey Mwanri kumkataa na kumtaka mhandisi wa ujenzi katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Atu Mwaipyana kuwasilisha vyeti vyake vya elimu ya sekondari hadi chuo alichosomea taaluma hiyo ,mapya zaidi yazidi kuibuka dhidi ya mhandisi huyo mtanzania limedokezwa.

Wakizungumza mtandao huu kwa sharti la kutotaja majina yao kutajwa kwa usalama wa kazi zao mmoja kati ya makandarasi ambao wamepata kufanya kazi ya ujenzi wa miradi mbali mbali ikiwemo ya barabara katika wilaya hiyo ya Kilolo wameibuka na kupongeza hatua zilizochukuliwa na naibu waziri huyo na kudai kuwa miradi mbali mbali ilikuwa ikifanywa na mhandisi huyo kwa kuingia mikataba ya kirafiki na baadhi ya makandarasi

Kwani walisema hata vyoo vya stendi ya Ikokoto Ilula ambavyo Mwanri alipinga ujenzi wake kazi hiyo ilifanywa na mhandisi huyo kwa kushirikiana na dada mmoja mbaye ni rafiki yake wa karibu na kuwa kazi hiyo imetumia zaidi ya shilingi milioni 40.

Hivyo walisema kuwa hawaoni sababu ya mhandisi huyo kuficha mkandarasi aliyefanya kazi ya ujenzi wa choo hicho kwani kwa kawaida kazi yoyote katika Halmashauri inayozidi zaidi ya shilingi milioni 5 ni lazima tenda itangazwe na watu wenye sifa waweze kuomba tenda husika ila katika ujenzi wa miradi mbali mbali imekuwa ikifanywa kiholela bila ya tenda kutangazwa.

"Pamoja na naibu waziri kumwagiza kuonyesha vyeti vyake vya elimu bado haitoshi kwani mhandisi anapaswa kutaja jina la mkandarasi aliyefanya ujenzi wa vyoo vya stendi na baadhi ya barabara za wilaya ya Kilolo ....kiukweli ipo miradi mingi ambayo imefanywa na mhandisi huyo kwa kutumia jina la kampuni ila anajilipa yeye na fedha kidogo kumlipa mkandarasi aliyemkodishia jina.....tunaomba wanahabari kujaribu kuwatembelea makandarasi ili mpate maoni yao na baadhi yao wanaweza kuwapa hata BOQ za miradi hiyo"

Kwa upande wake mhandisi huyo wa wilaya ya Kilolo Atu Mwaipyana akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana juu ya tuhuma hizo alisema kuwa hazina ukweli kwani miradi yote inafanywa na Halmashauri kwa kuzingatia taratibu zote na kuwa hakuna mradi wa mtu mmoja .

Akitolea mfano barabara mpya ya Kilolo yenye urefu wa kilomita 2.5 ambayo imejengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 72 na naibu waziri huyo kuikataa kwa madai haina kiwango alisema kuwa kampuni iliyofanya kazi hiyo ni kampuni ya Datwa Ltd iliyopo mjini Iringa .

Mwaipyana alisema kuwa katika ujenzi wa vyoo vya stendi kazi ilifanywa na mafundi wa mitaani ambao wamepata mafunzo kupitia mradi wa VPTP kwa ajili ya ujenzi .

Hata hivyo alisema kuwa kilichofanyika katika suala lake hilo ni kugeuzwa kondoo wa kafara kwa niaba ya Halmashauri hiyo .

Mhandisi huyo ambaye ni pekee katika mkoa wa Iringa aliyesajiliwa katika bodi ya makandarasi Tanzania ,alidai kuwa elimu yake si ya kufoji bali ni elimu aliyoipata chuo japo zipo taarifa kuwa katika wilaya ya Kilolo mhandisi huyo alipangiwa na ofisi ya TAMISEMI.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: