KABWE ZUBERI ZITTO, MP
KIGOMA KASKAZINI
KIGOMA KASKAZINI
---
1.
Baadhi
ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa
kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais’. Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa
chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni
tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais.
Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama changu,
wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu
lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.
2.
Kwa
hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu
kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba
hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka
40 akose sifa za kuwa Rais. Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma
shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu
niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate
fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili
yangu. Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya
kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi
ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine
wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika
usukani wa nchi yetu. Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika
uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.
3.
Tunapojiandaa
kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa
bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa
wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.
Dar
es Salaam
29 Februari 2012
Toa Maoni Yako:
0 comments: