Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba a.k.a Ruge wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.
 Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo).
----
Vicky Kimaro
BAADA ya mvutano wa muda mrefu uliojaa kauli zisizopendeza kusikika mbele ya jamii, hatimaye Mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi jana walishikana mikono ikiwa ni ishara ya kumaliza tofauti zao.


Shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida, Tundu Lissu kwa kufanikisha kuwashawishi 'wababe' hao katika tasnia ya filamu kumaliza tofauti zao.


Ruge na Mbilinyi 'Sugu', walikuwa kwenye ugomvi kwa kipindi kirefu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgongano wa kimaslahi ambao ulisababishwa na mradi wa Malaria uliojulikana kama 'No more'.
Aidha, sababu nyingine ni studio iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete na kupewa THT pamoja na hatua ya kituo cha Radio cha Clouds kutopiga nyimbo za baadhi ya wasanii na malipo finyu kwa wanamuziki wa ndani tofauti na wale wa nje.


Akizungumza kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Waziri Nchimbi alisema kuwa mchakato wa kumaliza tofauti za Sugu na Ruge umekuja baada ya kikao cha bunge lililomalizika hivi karibuni.


"Kwenye kikao cha bunge lililopita nilitoa taarifa kuhusu mkutano wa vijana nilioudhuria Kampala na jinsi vijana wanavyotakiwa kutoa tofauti zao na kufanya shughuli za maendeleo na kuleta tija kwenye taifa.


"Baada ya kikao kile, Sugu alinifuata na kuniambia taarifa niliyotoa ni nzuri na alidhani ningemwambia kwanza yeye kabla ya kuisema kwenye bunge, kupitia taarifa ile Sugu akaomba nimkutanishe na Ruge na kumaliza tofauti zao," alisema Nchimbi.


"Nilimuliza Sugu kama kweli ana dhamira ya dhati, akaniambia ndiyo. Baada ya Bunge tulifanya vikao mbalimbali na hiki cha leo ni cha mwisho, wapatanishi nikiwa mimi na muheshimiwa Lissu. Nashukuru jitihada zetu zimezaa matunda na leo ukurasa mpya unafunguliwa."


"Katika upatanishi pande zote mbili ziliridhika kuwa msingi wa mgogoro wao ni kila upande kuwa na kundi la wasanii na kuamini kuwa upande mmoja hautendei haki upande mwingine.


"Pande hizo pia ziliridhika kuwa mgogoro baina yao unajenga uhasama na utengano mkubwa miongoni mwa wasanii ambao wanapaswa kuungana kudai na kusimamia maslahi yao," alisema Nchimbi.


Akitangaza makubaliano yao Nchimbi alisema Ruge na Sugu wamekubaliana wanamaliza mgogoro na uhasama baina yao. Watashirikiana kufanikisha mambo yote yanayohusu muziki.


Kwa upande wa Ruge alisema: "Namshukuru Lissu, na waziri Nchimbi kwa hatua tuliyofikia, sisi tuna ushawishi mkubwa kwa jamii hasa vijana, tunadhoofisha sekta ya sanaa, aliyosema waziri ni sawa nimemaliza tofauti na Sugu kwa moyo mweupe bila shinikizo lolote, tumefunga ukurasa wa zamani na tunaanza ukurasa mpya."


Wakati Ruge akisema hayo, Sugu alisema: "Tulikuwa katika vita, na vita lazima ifike mwisho, labda kama vita hiyo haina malengo, suala ilikuwa ni maslahi na haki ya wasanii tumeshakaa tukazungumza kwa moyo mweupe sasa hivi Fleva Unit na Tuma ni kitu kimoja, tutakaa na kuunganisha vyama hivyo na kuwa chama kimoja ambacho kitafanya shughuli za Wasaniii na Studio iliyotolewa na Rais itarudi kwenye mikono sahihi." alisema Sugu muhasisi wa kundi la Vinega walitamba na albumu yao ya Anti Virus.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

2 comments:

  1. Wagombanao ndio wapatanao, good for them

    ReplyDelete
  2. afadhali............bifu bifu sio nzuri kabisa katika maisha ya mwanadamu, nimefurahi sana kusikia hili, nawaombea mema ili upatano wao uwe wa kweli na si wa mdomoni tu. Hongera sana Ruge & Mbilinyi kwa uamuzi mliofikia. Mbarikiwe

    ReplyDelete