Na Mwandishi wetu
Timu ya Soka ya Villa Squad Fc leo inataraji kujitupa uwanja wa Chamazi kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Azam fC ili kujiwinda na raundi ya pili wa ligi kuu Tanzania Bara.
Frank Mchaki |
Afisa habari wa Villa, Andrew Chale, alisema mchezo huo wa kirafiki utakua ndio wa mwisho na baada ya hapo timu inatarajia kuingia kambini kujiwinda na ngwe hiyo ya lala salama.
Katika kikosi hicho kinachonolewa na kocha mkuu Abib Kondo, kipo fiti asilimia 90 na kinatarajia kufanya makubwa tofauti na kile cha awali ambacho karibu wachezaji wengi walibadilishwa na kuajiriwa wapya.
"Villa Squad FC ya sasa si kama ile ya awali hii ina kila kitu wachezaji wana hali ya kuonyesha maajabu hivyo tunaomba wadau wajitokeze kwa wingi kuja kuishangilia Villa katika mchi hii ya mwisho ya kirafiki sambamba na kujitokeza kuichangia msaada wa hali na mali" alisema Chale.
aidha kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Villa , Frank Mchaki alisema kua uongozi mzima kwa kushirikiana na kamati ya ligi ya timu hiyo umejipanga kuakikisha Villa inasimama bila kuteteleka na kuonyesha soka la uhakika na kuiletea heshima mkoa wa Kinondoni ulio na timu hiyo pekee ligi kuu.
Mchaki alitoa rai kwa wadau mkoa wa Kinondoni kujitokeza kuipa tafu timu hiyo ambayo imedhamiria kuonyesha maajabu sambamba na kuakikisha inapigana kiume ilikuendelea kubaki ligi kuu. "Tunaomba wadau wa Kinondoni na Tanzania kwa ujumla, kujitokeza na kuisaidia Villa iendelee kubaki ligi kuu kwani kikosi sasa kimebadilika na kinauuwezo mkubwa kuonyesha maajabu kipindi hichi cha lala salama" alisema Mchaki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: