Hivi huu usafiri wa boda boda ni salama kwa utumiaji au ni kutaka kuwahi muda katika shughuli zako tu? uwapi usalama wako?
Vibajaji vikiwa kwenye foleni vikisubiri wateja mapema jana njia panda Kawe chini. Uwingi wa hivi vibajaji ambavyo vimetapakaa kila kona ya jiji umekuwa ukirahisisha usafiri kwa abiria, ambao baadhi yao wamekuwa wakilalamikia huduma ya Taxi kwamba wanatoza hela (nauli) nyingi, hivyo wamekuwa wakipendelea zaidi vibajaji kusafiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Aidha, baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa ujio wa Vibajaji na Boda Boda (pikipiki) zimeidhoofisha kwa kiasi fulani biashara ya usafiri wa Taxi.
"Kwa wingi wa vibajaji, wingi wa boda boda, wingi wa taxi, wingi wa dala dala na wingi wa magari binafsi na pikipiki binafsi, kuna haja serikali kuangalia njia nyingine za usafiri mjini kupunguza wingi wa migongano ya magari, foleni na kuendeleza miundo mbinu mjini. Pengine iwapo jiji letu la Dar es Salaam tutashindwa kukabili jambo hili kwa kiasi fulani, kuna haja ya kuwaita MetroCount kwa kuanzia na mengine kufuatia." Angalia jinsi hiyo ilivyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: