Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi ishirini na nne, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) kama washindi wa kwanza wa kila siku ambao wamepatikana katika promosheni inayoendelea ya “Zamu yako Kushinda.”
Halikadhalika washindi wengine arobaini na nane wamezawadiwa kompyuta aina ya laptop za Samsung. Washindi wamepatikana katika kipindi cha siku 24, na jumla ya fedha zilizotumika kulipa washindi mpaka leo ni Shilingi za Kitanzania milioni 204.
“Tumeridhishwa na namna ambavyo promosheni inaendelea,” alisema Alice
Maro, Meneja Mahusiano wa Tigo. “Bado tunazawadi nyingi za kugawa, kwa
hiyo tunapenda kuendelea kuwasihi wateja wetu kushiriki,” alisema.
Baadhi ya washindi wa Tsh. 4,000,000/- ni Juliana Deus (Tabata); Esther
Elia (Mbezi Beach); Andrew Mwemezi (Mbeya); Petronila Mtatiro (Ukonga)
na Julius Yohana Mlacha (Ubungo).
Baadhi ya washindi wa laptop ni Dini Kaikai (Ilala); Benjamin Jumbe
(Dodoma); Mwanate Abdallah (Mbagala); Hezron Chacha Kehongo (Mbezi
Beach) na Omar Msuya (Buguruni); George Kessy (Ngara,Kagera).
Washindi wengine wametoka sehemu mbalimbali nchini kama Bukoba, Mwanza,
Morogoro, Dodoma, Mtwara, Lindi, Tanga, Moshi, Arusha, Rukwa, Singida
and Pwani.
Ili kushiriki mtumiaji wa Tigo anatakiwa kutuma neno “TIGO” kwenda
15571. Gharama kwa kila ujumbe ni Tsh 450. Washiriki wanatakiwa
kujikusanyia pointi nyingi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kujishindia
zawadi. Washiriki pia watazawadiwa zawadi za kutuma ujumbe wa bure
kutoka Tigo kwenda mitandao yote Tanzania.
Watumiaji wa mtandao wa Tigo wenye umri chini ya miaka 18, hawaruhusiwi
kushiriki. Promosheni hii ni kwa ajili watumiaji wa Tigo watanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments: