Baada ya shughuli nzima ya maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special,kinachorusha na redio ya Wapo FM,wageni waalikwa walipata picha ya pamoja kama ukumbusho muhimu kwao, nje ya jengo la mikutano la Taasisi ya Maendeleo ya Vijana (UVIKIUTA), iliopo Chamazi-Mbagala jijini Dar.
 Keki tuliii safi kabisa.
Mmoja wa wageni kutoka meza kuu,Wakili wa Kujitegemea Bw. Emanuel Makene akikata keki kwa ajili ya kulishwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya kipindi hicho ambacho kimekuwa kikipendwa na kusikilizwa sana wanajamii.
 Mtangazaji wa Wapo FM, Dada Benedict Mrema akichombeza hapa na pale,huku muasisi wa kipindi cha Weekend Special, Antony Joseph akitaka kuwalisha wageni waalikwa keki iliondaliwa maalum kwa maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi hicho tangu kuanzishwa kwake.
 Keki ikigaiwa kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo.
 Mmoja wa wasanii  kutoka Taasisi ya Maendele ya Vijana (UVIKIUTA) akiwaburudisha wageni waalikwa
Mmoja wa vijana wajasiliamali akifafanua kuhusiana na matatizo mbalimbali wanavyokumbana nayo katika shughuli zao mbalimbali za kila siku za ujasiliamali.
Mtangazaji wa Wapo FM redip, Dada Ritha Chaula akisoma hotuba fupi kuhusiana na maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special,mbele ya meza kuu na wageni waalikwa mbalimbali waliofika. Kipindi hicho hurushwa kila siku ya jumamosi kuanzia saa 8 mchana mpaka 11.30 jioni kikiwa na lengo la kuelimisha na kuipasha jamii maovu yanayotendeka, namna ya kukabiliana nayo na kuyaepuka, sambamba na hayo kipindi hicho pia huibua na kutangaza matukio ya unyanyapaa, unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji na ulawiti, kuwapa vijana elimu ya stadi ya maisha ili waweze kujitambu,kujiamini na kujiajiri katika kuyakabili maisha kiuchumi, kuibua migogoro ya ndoa, kupata elimu ya namna ya kutatua na kupata suluhisho la kudumu.


 Wadau wakifautilia kongamano wakati likiendelea.
Baadhi ya Watangazaji wa Wapo Fm redio wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri ndani ya ukumbi,wakati kongamano la vijana likiendelea.Sho ni DadaRitha Chiwalo, Benedict Mrema na mdau wa Wapo FM.
Pichani kulia ni Dada Faines Mwakatobe kutoka Chuo Kikuu Huria cha jijini Dar akiwatafsiria baadhi ya Walemavu wa kutosikia,ambao pia wameshiriki katika Maadhimisho ya miaka mitano (5) ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na redio Wapo FM, kila siku ya jumamosi. Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kongamano la vijana ambalo lilijadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, ajira, elimu na mambo mengineyo.
Baadhi ya wadau wa kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM ambao pia wameshiriki katika Maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na redio Wapo FM cha jijini Dar, kila siku ya jumamosi.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini mijadala iliyokuwa ikitolewa kwenye maadhimisho hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
 Waimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili kutoka kundi la Double E likitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Mtangazaji wa kipindi cha Wikend Special kinachorushwa na redio ya Wapo FM, ambacho leo kinaadhimisha miaka 5 tangu kuanzishwa kwake, Bw. Antony (kulia), akiwatambulisha viongozi wa vikundi  mbalimbali mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) waliofika kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika leo kwenye viunga vya UVIKIUTA-Chamazi jijini.
Mwakilishi kutoka  TYC, Bw. Nyakia Ally akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa (ambao kwa asilimia kubwa ni vijana kutoka sehemu mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Special Wikend kinachorushwa na redio ya Wapo FM, anayefuata ni Wakili wa Kujitegemea Bw. Emanuel Makene, Dr. Nassoro Ally Matuzya kutoka hospitali ya Mwanyanyamala, Mmoja wa wakilishi kutoka chuo kikuu UDSM, Bw. Edward Daniel na shoto ni Mwendesha kipindi cha Wikend Special Bw.Antony Joseph.
Kongamano likiendelea kwa umakini kabisa.
Mmoja wa wanaharakati vijana, Dr. Nassoro Ally Matuzya kutoka hospitali ya Mwanyanyamala akifafanua jambo ikiwa ni sehemu ya kongamano la vijana la kuelimishana kuhusiana na mambo mbalimbali zikiwemo changamoto wanazokabiliana/kumbana nazo katika mfumo mzima wa maisha yao ya kila siku.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Pius Senyagwa sambamba na wasanii wengine wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
Makofi ya hapa na pale yalikuwepo kutoka kwa wageni waalikwa.
Baadhi ya vijana walioko kwenye Taasisi ya Maendeleo ya Vijana (UVIKIUTA), kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mijadala mbalimbali iliokuwa ikizungumzwa kwenye kongamano lililoendana sambamba na maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na redio ya Wapo FM jijini Dar, maadhimisho hayo yamefanyika kwenye viwanja vya taasisi hiyo huko Chamazi-Mbagala jijini Dar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: