Pichani ni Said Tamimu Ally
Ndugu zangu
Natoa shukrani zangu za dhati na kwa niaba ya familia ya ndugu Said Tamimu Ally. Nashukuru sana kwa wote waliotoa michango yao ya mali na hali kwa ajili ya kumsaidia ndugu yetu Tamimu. Shukrani pekee ziwaendee ndugu walioko UK, Norway, Muscat, Dar es salaam, Tabora, Arusha na sehemu nyinge nyingi kwa msaada wao wa hali na mali ikiwemo ushauri na kutoa pole.
Pili ningependa kuwajulisha kuwa kaka Tamimu siyo mtoto nadhani nilipotuma kwenye blog nilisahau kutaja umri. Huyo ni mtu mzima mwenye mtoto mmoja wa darasa la saba. Mimi siyo mzazi ila nilimfahamu wakati anapata matibabu hospitali ya KCMC Moshi. Baada ya kumuona anatatizo niliendelea kunfuatilia mpaka alipo pata referal kwenda Ocean Road Hospital. Kwa sasa hali yake inaendelea kuzorota kwani ameniambia alikwisha maliza kupata mionzi 20 ambayo ameandikiwa pale Ocean Road Hospital, anakwenda na kurudi siku ya clinic.
Nashukuru kwa mawazo ya wengi nimeweza kufungua account benki ya NMB Magomeni ambayo msimamizi ni mdogo wake aitwae Fatuma Tamimu. Ametoa idhini account ifunguliwe kwa jina la mdogo wake wa kike kwani mtoto wake ana umri wa chini ya miaka 18. Kwa wale wote waliotumia M-Pesa,Tigo pesa na Western Union nimekabidhi pesa kwa ndugu Tamimu. Kwa niaba yake natoa shukrani za dhati, asanteni sana. Lakini kwa vile tumefungua accout basi watakaoguswa watumie account number hii
20510000732
NMB Magomeni Branch
Fatuma Tamimu
Kama nilivyosema hali ya afya yake siyo nzuri na namba yake ya simu ni hii 0657-584336 anaweza kuzugumza unaweza kumpigia na kuongea naye. Mwenyezi Mungu awazidishie wote
Asante sana
Anna Sangai.
Toa Maoni Yako:
0 comments: