Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chama Cha Mapinduzi-CCM) na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mh. Jeremia Sumari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa Kansa ya kichwa. Habari kamili tutaendelea kuwaletea.

Marehemu Sumari ni mbunge wa pili kwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufariki kwa mwaka 2012, baada ya kutanguliwa na mbunge wa viti maalum Chadema Bi. Regia Mtema aliyezikwa jana tarehe 18.1.2012 nyumbani kwao Ifakara, Morogoro ambapo mazishi yake yaliongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: