Shirika la Umeme Tanzania limekuwa likipata changamoto kubwa kuhusiana na mfumo wa usomaji wa mita za umeme na uhakika wa Ankara za umeme linazowapa wateja wake.
Kutokana na changamoto hizi shirika limefanya jitihada mbalimbali ili kuboresha huduma, mojawapo ya jitihada hizi zilifanikisha kuanzishwa kwa mfumo wa malipo ya umeme kabla ya matumizi yaani LUKU.
Mita za Luku zilifanikisha kupunguza changamoto ya usomaji mita na uhakika wa Ankara kwa wateja wenye matumizi madogo ya umeme. Hata hivyo changamoto hizo ziliendelea kuwa kero kwa wateja wenye matumizi makubwa ambao kiufundi hawawezi kutumia mita za LUKU.
Mnamo mwaka 2008, jitihada endelevu za shirika zilifanikisha majaribio ya matumizi ya mita zinazosomwa kwa kutumia komputa mita hizi hujulikana kwa jina la AMR yaani “Automatic Meter Reader”. Kufuatia mafanikio ya maradi wa majaribio (AMR Pilot Project), mnamo mwaka 2009 TANESCO ilianza kufunga mita za AMR kwa wateja wakubwa (Tariff 2 na Tariff 3) na wateja wa kati (Tariff 1 – Three phase).
Teknolojia ya AMR inawezesha kusoma na kurekodi matumizi ya umeme kila saa kwa usahihi mkubwa. Mita za AMR hupeleka taarifa za usomaji wa mita kwenye komputa za shirika zilizopo makao makuu kila saa. Mfumo wa kompyuta za AMR hupokea na kuratibu taarifa za matumizi ya umeme kutoka kwenye mita ya mteja na kuandaa taarifa mbalimbali.
Mteja anayetumia mita za AMR anaweza kupata taarifa ya matumizi yake ya umeme wakati wowote anapohitaji taarifa hizo kwa kutomia tovuti ya Shirika la Umeme Tanzania (www.tanesco.co.tz).
Huduma hii imerahisisha upatikanaji wa takwimu za matumizi ya umeme na hivyo kumwezesha mteja kudhibiti matumizi yake ya umeme.
Shirika pia linanufaika kwa kupunguza gharama za usomaji mita, kupunguza makosa ya kibinadamu katika usomaji mita na uandaaji wa Ankara, kudhibiti wizi wa umeme na kuhakikisha taarifa za matumizi ya umeme uliosambazwa zinapatikana kwa uhakika na kwa wakati zinapohitajika.
Pamoja na manufaa yanayopatikana kutokana na matumizi mita za AMR, shirika bado linaendeleza jitahada za kuboresha usomaji wa matumizi ya umeme na uhakika kwa ankara. Shirika limefanikiwa kupata teknolojia ya kisasa zaidi ya mita za AMR ambayo itaanza kutumika mwaka huu (2012). Mita hizi mpya zitaunganisha teknolojia ya AMR na ile ya LUKU ambapo mteja atalipia umeme kabla ya kutumia na shirika litaweza kupata taarifa ya matumizi ya mteja pamoja na mwenendo wa mita kwa wakati. Hii itasaidia kuongeza mapato ya Shirika na kudhibiti upotevu wa umeme. Mita hizi zitafungwa kwa wateja wa kati (Tariff 1 Three Phase).
Shirika linawahakikishia wateja kuwa teknoljia ya AMR ni ya kisasa na inahakikisha usahihi katika usomaji wa matumizi ya umeme.
Teknolojia hii hutumiwa na mataifa mengi hapa duniani ikiwemo USA, Umoja wa Ulaya, Uchina, Amerika ya Kusini na nchi mbalimbali za Afrika. Hapa Afrika ya Mashariki, Tanzania ni nchi ya pili inayotumia mita za AMR. Tayari jirani zetu Kenya wanatumia mita hizi na wanafurahia manufaa yake.
Badra Masoud
Meneja Mahusiano
ningependa...kufaham...namna..ya...kusoma...units...zilizobaki...kayika..mita..yangu...
ReplyDeletesababu..kwa..kias..flani...hz..mita...zinachanganya...kuna...wakati...meter..ukiingalia...inaonyesha...namba(units)...tatu...tofauti...napata...ugumu..kujua...zipi...ni...units...halis...na...hiz..zingine...zinakuwa....zinawakilisha...nini...
**some..one...to..help..me..please..***