Waandaaji wa Kitchen Party Gala, Dina Marious (kushoto) akiwa na Vida Mahimbo walipokutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam kuzungumzia Kitchen party gala.Tukio ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Danken house mikocheni ambao ndiyo ukumbi rasmi wa shughuli hii jumamosi ya tarehe 28 january.
---
Wasichana na
wanawake wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo
zinapelekea kushindwa kusimama katika mahusiano yao. Teknolojia, mwamko wa
elimu,wanawake kumiliki biashara binafsi, kazi, wazazi hawahusishwi, kila mtu
mjuaji, kujisahau n.k
Matokeo yake talaka
nyingi na mahusiano kuvunjika sasa tunataka kumkumbusha mwanamke wajibu wake na
nafasi yake katika mahusiano. Ajitambue.
Msimu wa pili
Eneo hili limelenga
kukuza ujuzi wa mwanamke katika Nyanja za kijamii zaidi. Kupitia
eneo hili mwanamke atajifunza mambo mbalimbali kiasili na kisasa ambayo
mwanamke anaengia au aliyeko au anaetegemea kuingia katika mahusiano na
ndoa. Mambo kama malezi ya watoto, nafasi yake katika jamii umuhimu
kujiamini na mengineyo.
Wazo hili limekuja
mara baada ya kuona kwamba ule muda wanawake wanaopata kuongea mambo haya
kwenye kitchen party ni mchache na hautoshi kumfahamisha mwanamke
mambo yote muhimu. Mambo ambayo ni lazima ayajue au hata kama anayajua
kutokana na pilika pilika za maisha anajisahau.
Tukio hili
kufanyika jumamosi hii ya tarehe 28 January 2012. Kuanzia saa nane mchana mpaka
saa mbili usiku katika ukumbi wa Danken house uliopo mikocheni kwa warioba.
Watoa mada ni
watu wenye uwezo katika swala zima la uelimishaji.
Aunt sadaka; Ni
mwana saikolojia aliyebobea katika maswala ya wanawake na watoto.Ana
uwezo katika Nyanja hii ambao umetokana kielimi na uzoefu wa kukutana na
kesi mbalimbali amabazo zinazo mguza mwanamke hivyo kuweza kuwa funzo kwa
wengine.
Bi Chau: Ni mwanamke ambaye mbali na kuwa katika fani ya sanaa kwa muda mrefu
wamekua wakito amafunzo kwa wanawake tokea muda mrefu. Mafunzo ya
mahusiano, ndoa na familia kwa ujumla.
Mama Victor; Ni
mtumishi wa Mungu katika dini ya kikristo ambaye anaelimisha wanawake kwa
mafunzo ya kidini. Anafundisha mwanamke kujitambua vile mungu amempa uwezo
wa kuitumikia jamii yake kama mlezi na kiongozi.
Kwa ufupi hawa ndio
wakufunzi katika tukio letu hili la women in Balance jumamosi hii katika msimu
wa pili.
Burudani
itatolewa na Nyota Waziri.
Huu ni mkakati wa
mwaka mzima huu 2012 na tutakutana kila mwezi mpaka mwezi march ambapo ratiba
itabadilika na wanaume kuhusishwa.
WADHAMINI WETU WA
SIKU HII NI BAILEYS
(kinywaji), MGen Insuarance, Cocacola, Cooperate Image na Clouds Fm.
IMETOLEWA NA
MRATIBU WA WOMEN IN BALANCE.


Toa Maoni Yako:
0 comments: