Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Bwana Jeseph Kusaga wakisaini mikataba mkataba wa majaribio wa muda mfupi na kampuni ya Prime Time Promotions kwa ajili ya kuratibu, kusimamia na kuhamasisha mechi yake dhidi ya timu ya Zamalek ya Misri iliyopangwa kufanyika Februari 18 jijini.
Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Bwana Jeseph Kusaga wakibadilishana mikataba mara tu baada ya kusainiwa na pande zote mbili.
Picha ya pamoja mara tu baada ya Shughuli kumalizika
Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na Uchumi ya Yanga Mr Rupia, Katibu mkuu wa Yanga Celestine Mwesigwa na Mwenyekiti Lloyd Nchunga wakifurahia mara tu baada ya kutiliana saini mkataba na kampuni ya Prime Time Promotions wa kuisimamia mechi yao dhidi ya Zamalek ya Misri.
---
WAWAKILISHI wa Tanzania Katika Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imesaini mkataba wa majaribio wa muda mfupi na kampuni ya Prime Time Promotions kwa ajili ya kuratibu, kusimamia na kuhamasisha mechi yake dhidi ya timu ya Zamalek ya Misri iliyopangwa kufanyika Februari 18 jijini.
Mkataba huo umesainiwa jijini Dar Es Salaam huku Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga akisema kuwa Prime Time Promotions ambayo ni kampuni tanzu ya Clouds media Group pia itafanya kazi ya kutafuta wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mechi hiyo.
Nchunga alisema kuwa kampuni hiyo kwa sasa ndiyo itakuwa inafanya uratibu wa shughuli zao mbali mbali hususani za mechi na kama watafanikiwa katika mechi dhidi ya Zamalek, basi wataingia mkataba mnono zaidi ambao utawawezesha kuratibu mechi zao za Ligi Kuu ya Tanzania.
Alisema kuwa hiyo ni mikakati yao ya kuhakikisha wanafanya vyema katika mechi hiyo na kufuta uteja wa timu yao dhidi ya timu za Misri na Uarabuni kwa ujumla.
“Hii ni mikakati yetu ya kufanikisha mchezo huo na kushinda na wala si matokeo tofauti na hayo, kwa hivi sasa tumekwisha kamilisha malipo ya mishahara na madeni ya wachezaji ambao kwa sasa wanafikiria zaidi mechi za ligi kuu ya mechi dhidi ya Zamalek,” alisema Nchunga.
Aliongeza kwa kuwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa na utulivu wa hali ya juu kayika kufanikisha mechi hiyo na michezo ya ligi kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Prime Time Promotion, Joseph Kusaga alisema kuwa hatua ya kufanya kazi na Yanga ni moja ya mikakati yao ya mwaka huu katika maendeleo ya michezo nchini.
Kusaga alisema kuwa wanamikakati mingi kwa timu za taifa na za vijana huku wakielekeza nguvu katika soka la vijana wa shule za msingi na sekondari.
Alisema kuwa pia wanatarajia kufanya kazi na timu ya Simba SC katika mchezo wao dhidi ya Kiyovu ya Rwanda katika michuano ya Shirikisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments: