Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira Bw. Abdulkarim Shah akizungumza wakati wa kikao watendaji wa Ofisiya makamu wa Rais Mazingira Kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa. Naibu Katibu Mkuu Ofisiya makamu wa Rais Eng Ngosi Mwihava na Bi zakha Megji. (Picha na Maktaba).
---
---
Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho Tanzania.
Makumbusho ya Taifa imeshauriwa kutunza kumbu kumbu muhimu za urithi unao shikika na usio shikika ambao hauja hifadhiwa hadi sasa na ukiwa hatarini kupotea ili ziweze kunufaisha vizazi vilivyopo na vya baadae.
Ushauri huo umetolewa na Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilipo tembelea makumbusho ya Taifa ili kujionea Shughuli mbali mbali za kimakumbusho ukiwemo mradi mkubwa wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam uliofunguliwa mwishoni mwa mwaka jana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu CCM Dodoma, Mh Mariam S. Mfaki, alipotaka kujua kama Makumbusho imefanya jitihada zozote za kuhifadhi kazi na taarifa muhimu za wasanii walio liletea sifa Taifa hili akiwemo Hayati Mzee Moris Nyunyusa, Dr Paul Msemwa. Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamauni alijibu kuwa Makumbusho imesha fanya jitihada hizo kwani kabla Mzee Moris Nyunyusa hajafariki alisharekodiwa kwa njia ya sauti na video na hata Mzee Nyunyusa kuichangia Makumbusho Ngoma zake tatu kati ya zile kumi na mbili alizokuwa akizipiga, Aidha wasanii kama Marehemu Tinga Tinga kazi zao na taarifa zinatakiwa zikusanywe.
Nae Mbuge wa Jimbo la Matemwe Zanzibar Mh Kheri Amer aliishauri makumbusho ifanye utafiti wakina kuhusu historia muhimu zinazo husu utawala wa kisulutani ulio husisha Tanzania Bara na Visiwani ili taarifa hizo ziweze kuwasaidia watanzania kuelewa vyema mahusiano hayo kwa minajili ya kuuimarisha Muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Pamoja na Kuupongeza Uongozi wa Makumbusho kwahatua mbali mbali za kimaendeleo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Mafya Mh Shahalishauri uongozi wa Makumbusho kuandaa Programu ya pamoja kati ya Makumbusho zilizopo Zanzibar na Tanzania Bara ili kuimarisha mahusiano ya kimuungano kama ilivyopo sasa katika sekta mbali mbali za Utalii.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Tanzania, Bw Jackson Kihiyo, aliishukuru kamati hiyo kwa kutembelea Shirika la Makumbusho ya Taifa na kwa michango ya wanakamati na kuahidi kuwa Makumbusho itayatekeleza yaleyote yaliyo shauriwa na kamati hiyo.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira walipata nafasi ya kutembelea kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na cha Kijijicha Makumbusho ambapo walipata nafasi ya kujionea shughuli mbali mbali za Makumbusho hizo zikiwemo za Uhifadhi, Uelimishaji, Uridhishaji kwa kupitia kumbi mbali ukiwemo ule wa Kisasa wa Maonesho ya Sanaa za Jukwaani.


Toa Maoni Yako:
0 comments: