Mh. Pindi Channa
Kamati ya  kudumu ya bunge ya sheria, Katiba na Utawala Bora imesema imeridhishwa na miradi yote ya maendeleo iliyotekelezwa na mfuko wa taifa wa maendeleo ya jamii TASAF katika wilaya za Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya kamati hiyo kutembelea wilaya hizo na kukagua miradi ya TASAF mwenyekiti wa kamati hiyo Pindi Channa alisema kamati yake haina wasiwasi tena na utekelezaji wa miradi ya TASAF kwa kuwa miradi yote iliyoibuliwa na wananchi kupitia mfuko mfuko wa huo imekamilika na hakuna fedha zilizopotea.

Aidha mwenyekiti huyo pia ameushauri mfuko huo kuweka wazi jinsi fedha za miradi zinavyotumika ili kuondoa wasiwasi wananchi juu ya matumizi sahihi ya fedha za mfuko wa taifa wa maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladslaus Mwamaga alisema wakati mfuko huo utaendelea na utaratibu wa kuziwezesha familia maskini kupitia mfumo wake wa uhaulishaji mali ili wazee na watoto wanaoishi katika familia hizo kuweza kupata huduma mhimu ikiwemo
matibabu na lishe.

Miradi inayotekelezwa na TASAF katika wilaya za Rufiji na Mkuranga ni ujenzi wa vyumba vya madarasa  na  vyoo katika shule mabalimbali, zahanati, uanzishwaji wa vikundi vya kuweka akina na  kukopa, miradi ya kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na mpango wa kukuza uwezo
kujikimu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: