Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo Bw. Salum Mfaume na Bi. Happy Mgawe waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu wanaeleza jinsi ajali hiyo ilivyotokea.
---
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro baada ya gari la kampuni ya Upendo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka katika eneo la mkata barabara ya Iringa Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Adolfina Chialo akizungumza na Kajunason Blog kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi jioni baada ya gari la kampuni ya Upendo Lucky Star lenye namba za usajili T 510 AMZ likitokea Dar es Salaamu kuelekea Iringa ambapo dereva wake aliepuka kugongana uso kwa uso na lori na kujikuta likianguka mtaroni.

Chialo amewataja waliokufa kuwa wanaume wawili ambapo mmoja ametambuliwa kwa jina la Bw. Hamis Mbwana na kwamba dereva wa Lori amekimbia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: