Katibu Mkuu wa Umoja wa Masheikh na Wananzuoni Nchini, Sheikh Hamis Mataka (katikati) akisoma hotuba kabla ya kukabidhi msaada kwa ajili ya waathirika wa janga la mafuriko lililowakumba wakazi wa jiji Dar es Salaam, wakati walipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Masheikh na Wananzuoni Nchini, Sheikh Hamis Mataka (katikati) akikabidhi msaada wa Tshs. Mil. 12 kwa ajili ya waathirika wa janga la mafuriko lililowakumba wakazi wa jiji Dar es Salaam, wakati walipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutokea misaada kutoka kwa makampuni mbali mbali yaliyofika leo ofsini kwake jijin Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kupokea kutoka kwa kampuni ya Darbrew Ltd ambao ni watengenezaji wa Kinywaji cha Kibuku jijini Dar es Salaam pembeni yake ni Bw. Urban Shayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq akiongea na Kiongozi wa Care International in Tanzania Bw. Paul Barker wakati walipotoa msaada wao kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Bw. Hezron Lutengamaso wa Care International in Tanzania.
Kiongozi wa Mashirika ya Vijana nchini Nyakia Ally akiongea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq mara baada ya kutoa hotuba yake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq ini, akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa vijana wa Mashirika ya Vijana nchini, kushoto ni Kiongozi wao Nyakia ally na katikati ni mjumbe wa Bw. Sostenes Mitti.
Toa Maoni Yako:
0 comments: