Baada ya tume huru ya uchaguzi kumtangaza Joseph Kabila Kabage kama rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kiongozi wa chama cha upinza Etienne Tshisekedi naye amejitanga kuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Sasa hivi milio wa risasi inasikika katika Mji mkuu wa Kinshasa tagu jana. Mashirika ya haki za bidamu yamesema kuwa watu 6 wameuliwa kwa kupigwa risasi katika maeneo ya Mbijimai nako huko Kivu watu 3 wameuwawa akiwemo kiongozi wa shirika la raia Rutsuru Willy Mwabo.

Kulingana na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo Joseph Kabila ameshinda kwa asilimia 48, mpinzani wake mkuu Etienee Thisekedi akiwa na asilimia 32.33 na Vital Khemere naye akipata asilimia 7.74.

Mwaka 2006 alishinda uchaguzi wa kwanza tangu kumalizika kwa mgogoro wa miaka mitano na sasa anatarajiwa kuapishwa Desemba 20 kwa muhula wake wa pili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: