Picha hii niliipiga katika shughuli fulani hivi baada ya hao jamaa kama unavyowaona mwenyewe walipozidiwa  na pombe wakajikuta wanalala hapo hapo.
---
Hivi visa ni vya ukweli kabisa maana ndugu ama jamaa zetu wamediriki kujipa viburudisho na kuumbuka kwa ajili ya pombe.

1.Ilimkuta jamaa mmoja aliejikuta amelala kwenye tenga la nguo akifikiria ni chumba chake, alikunya kupita kiasi na kwa bahati mbaya wakati anarudi nyumbani kwake kulala akajikuta ameingia kwenye tenga la nguo na kulipasua kabisa akitegemea ni kitanda chake.


2.Akojoa sebuleni akidhani ni chooni, alijiona kama yupo chooni kumbe analimwaga kojo katikati ya sebule. Balaaah hii


3.Amelala chumba cha watoto akidhani ni kwa mkewe. Huyu mwanaume alijisahau na kujikuta amelala chumba cha watoto huku akidhani ni chumba chake akiwa na mke wake kumbe wala yupo kwenye chumba cha watoto.


4… Alala kwenye gari na kuzunguka na ruti zote mpaka alipozinduka mida ya saa 8 usiku akiwa yupo hoi kwenye daladala, nakujitia pombe alizokunywa.


5.Hii ndio noma akamtongoza mkwewe akidhani msichana wa miaka 18 tu, tena mbichi kumbe mkwe mwenye zaidi ya miaka 80. Jamani pombe noma.

Tujifunze kunywa pombe kwa raha lakini sio kujiletea karaha tu. Ulevi noma
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

2 comments:

  1. Kweli ulevi noma jama,chonde chonde walevi,funda moja tu chali.

    ReplyDelete
  2. Kweli ulevi noma jama,chonde chonde walevi,funda moja tu chali.

    ReplyDelete