Katika hali isiyokuwa ya kawaida mahabusu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ally Nuru maarufu kwa jina la Mwasa. Ametoa kali ya mwaka katika mahakama kuu ya mkoa wa Dodoma pale alipoavunja mlango wa mahabusu na kuingia chooni na kutoka na kinyesi cha binadamu na kujipakaa mwili mzima huku akilamba kinyesi hicho, akishinikiza kusikilizwa kwa kesi yake inayomkabili.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika mahakama kuu ya mjini Dodoma mara baada ya Ally Nuru na mahabusu wenzake kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusomewa kesi zao ndipo alipofanya kitendo hicho na kusababisha shughuli za mahakama kusimama kwa muda.

Ally Nuru maarufu kwa jina la Mwasa hakuishia kujipaka kinyesi bali pia alienda katika mlingoti wa bendera ya taifa na kuifungua na kusababisha bendera hiyo kufunguka huku Jeshi la Polisi wakijitahidi kumwagia maji ili aache kufanya hivyo.

Baada ya kujisalimisha alipelekwa kituo cha polisi kufanyiwa usafi na kurejeshwa mahakamani kujibu tuhuma za kufanya fujo, na uharibifu wa mali za mahakama. 
Pamoja na kutenda makosa yote hayo mahakamani na  mtuhumiwa huyo amekana mashitaka yote mbele ya hakimu mkazi Adrian Kilimi na kesi yake imeahirishwa hadi itakapotajwa tena kesho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: