Na Mwandishi wetu
MBUNIFU wa mavazi Irene Rwakatare juzi ameibuka kuwa mshindi katika shindano la wabunifu wa mavazi lililoshirikisha wabunifu 14 kutoka sehemu mbalimbali na wanamitindo 24 kutoka Vyuo mbalimbali vya Mjini Dodoma ambalo lilijulikana kwa jina la Uni Fashion Bash liliofanyika Royal Village mjini Dodoma .
IRENE alionekana kuwa mshindi baada ya majaji wanne kumpa kura kutokana na kile alichokionyesha kwenye shindano hilo na kujinyakulia kitita cha zawadi ya shilingi laki saba usiku huo wa juzi uliohudhuriwa na maelfu ya wanafunzi kutoka vyuo vyote vya mjini Dodoma.
Shindi wa pili katika wabunifu alikuwa Theresa Justo ambaye alijinyakulia shilingi laki tano,wa tatu Salim Twaha ambaye alipata laki tatu,wa nne Mary Mweleka alipata laki moja na watano Ally Mwenda ambaye pia alipata laki moja.
Upande wa wanamitindo aliyeibuka mshindi ni Respious Denis ambaye alijinyakulia zawadi ya shilingi laki tano na kufuatiwa na Nesia Kalatha ambaye alipata laki nne na wa tatu ni Prisila Mponega alipata laki tatu,wa nne Vakari Zuberi alipata laki moja na wa tano Miriam Mwaijange alipata laki moja pia.
Shindano hilo kwa ujumla lilikuwa la msisimko hivyo lilionekana kuleta upinzani hasa baina ya chuo na chuo hasa katika swala la wanamitindo kuona ni chuo kipi kitatoa mwanamitindo bora na msindi hivyo kufanya ushangiliaji kuwa wa hali ya juu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: