Mh Balozi na Mama Balozi wakifungua mziki.
 Mh Chabaka na Mchumba wake wakicheza.
 Mh Naibu waziri katika Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Aggrey Mwanri.
Muda wa kusugua visigino.
 Twanga Pepeta katika picha ya pamoja na viongozi.
 Mh Naibu waziri katika Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Aggrey Mwanri.
 Kila mtu akifurahia show ya Twanga Pepeta
 Kikazi zaidi.
 Club 2000 palikua hapatoshi.
 Makamuzi yakiendelea.
Mgeni Rasmi Mh Balozi Peter Kallaghe akifanya Toast.
---
Na Freddy Macha
 African Stars Entertainment Tanzania (Aset) ambao wanajulikana kwa jina la  “Twanga Pepeta” walikuwa  kivutio cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru London juzi Jumamosi.

Kikosi hiki cha watumbuizaji maarufu wa Kibongo kilikaribishwa na  Urban Pulse, Jestina George wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania mjini hapa.

Watanzania wa kila rika, nasaba na taaluma walifurika toka miji ya Leeds, Bristol, Birmingham, Northampton, Milton Keynes na vitongoji mbalimbali kufurahia vigongo vya bendi hili lenye makao makuu Mango, Kinondoni Dar es Salaam.

Ukumbi wa Club 2000 Banqueting Suite ulioko nyuma ya uwanja maarufu wa Wembley ulishuhudia tafrija hiyo wakati viongozi rasmi wa serikali walipofungua tafrija wakicheza nyimbo maarufu za Kitanzania kama ule wa mwanamuziki Salum Abdallah (“Wanawake wa Tanzania” na “Tujenge Nchi Yetu”) marehemu alizoimba mara baada ya Uhuru mwaka 1961.

Viongozi waliojumuika walikuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Balozi wa Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, naibu wake Mheshimiwa Chabaka Kilumanga na Ofisa Habari ndani ya ubalozi, Mheshimiwa Amos Msanjila aliyehamasisha wageni kwa kunyofoa kinywaji cha “champagne” mahsusi kuzindua maadhimisho.

Akiwakaribisha wageni Balozi Kallaghe alisema sherehe za miaka 50 ni idhinisho kuwa Tanzania ni nchi ya amani inayostahili kuwa fahari yetu sote. “Waangalie Waingereza wanavyoorodhesha tarehe na mida ya majengo yao muhimu. Kutambua na kusherehekea muda kamili wa matukio ya jamii ni jambo muhimu na la kawaida,” alikumbusha kiongozi huyo na kupigiwa makofi.

Kutokana na maombi mengi ya washabiki Twanga Pepeta itafanya Show ya pili siku ijumaa Tarehe 2 Desemba 2011 katika mji wa Milton Keynes kwenye ukumbi wa Golden Lounge, Unit 35 Barton Road, Bletchley Milton Keynes.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: