Ofisa Viwango wa Kampuni ya Tigo Pamela Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea kuhusu promosheni yao mpya ya 'Zamu Yangu' inayoanza kesho tarehe 1.12.2011 Dar es salaam pembeni yake ni Benedict Mponzi.
 Msimamizi wa Viwango wa Kampuni ya Tigo Benedict Mponzi (kushoto) akikazia mazungumzo wakati akielezea kuhusu promosheni yao mpya ya 'Zamu Yangu' inayoanza kesho tarehe 1.12.2011 Dar es salaam pembeni yake ni Ofisa Viwango wa Kampuni ya Tigo Pamela Shelukindo.
---
Tigo inawaletea wateja wake shindano liitwalo “ZAMU YAKO KUSHINDA” litakalochukua siku 82 ambapo washindi watazawadiwa TShs 4,000,000 kwa mshindi wa kwanza, wakati mshindi wa pili na wa tatu kila mmoja kompyuta ya Samsung aina ya Laptop. 

Ili kushiriki, mteja yeyote wa Tigo anatakiwa kutuma neno “TIGO” kwenda namba 15571 ambapo kila SMS itamgharimu mteja huyo Tsh450. Wateja wa Tigo ambao wana umri chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki. Shindano hili litakuwa na jumla ya washindi 246. 

Kampuni ya Tigo imeamua kuleta shindano ili kuwapa changamoto wateja wake na kutoa nafasi za kushinda zawadi kwa wale wa malipo ya kabla na ya baadae ambao walishiriki katika shindano lililopita. Washiriki wanatakiwa kutuma ujumbe mfupi kuanzia saa sita kamili usiku wa tarehe 30 November 2011 mpaka saa 11:59:59 usiku wa tarehe 19 February 2012. 

Mteja anayeshiriki kwenye shindano hili anatakiwa kujilimbikizia pointi nyingi iwezekanavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda. Mteja mwenye pointi nyingi kwenye shindano la “Zamu Yako Kushinda” atakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda kuliko mteja mwenye pointi chache.

Pointi zinapatikana kwa njia ya kutuma SMS kwenda namba 15571, ambapo mteja atapokea maswali mbalimbali ya chemsha bongo. Mteja akiyajibu maswali hayo kwa usahihi, atajipatia pointi kadhaa kulingana na swali alilojibu. Aina ya swali litakaloulizwa litategemeana na aina ya mchezo ambao mshiriki anacheza kwa mfano jiografia, uraia, michezo na kadhalika. Vilevile, baadhi ya washiriki watajishindia dakika za bure kupiga simu Tigo kwenda Tigo.

Kutakuwa na namba ya ziada, 15688. Namba hii itakuwa ikitumika na watumiaji wanaohitaji msaada au taarifa zaidi juu ya shindano hilo bila kutozwa gharama yeyote ile. Ili kupata msaada, mteja wa Tigo anatakiwa kutuma neno “help”, msaada au msada kwenda kwenye namba 15568. Pia washiriki wote wanaweza kutumia namba hii kuangalia salio la pointi zao kwa kutuma neno points, pointi au point. 

Zawadi ya kwanza ya TSh 4,000,000 itatolewa kwa mshindi mmoja kila siku, atakayechaguliwa kwa njia ya bahati nasibu. Zawadi ya aina moja haitatolewa zaidi ya mara moja kwa mshindi mmoja katika kipindi cha shindano hilo. Zawadi ya pili na ya tatu ya laptop aina ya Samsung pia zitakuwa zikitolewa kwa mshindi mmoja kila siku kwa kila zawadi. 

Aidha, zawadi ya pili na ya tatu nazo zitatolewa mara mmoja tu kwa mshindi mmoja katika kipindi cha shindano hili. Hii ina mana kuwa mshindi mmoja hawezi kushinda zawadi ya Sh milioni 4 mara mbili au Samsung laptop mara mbili katika shindano hili. Zawadi zitatolewa katika siku zote za wiki (Jumatatu mpaka Jumapili) za shindano hili.

Shindano ni la wazi kwa wakazi wa Tanzania na ni wateja wanaotumia mtandao wa Tigo wanaoruhusiwa kushiriki kisheria. Watanzania wanahimizwa kushiriki katika shindano hili kabambe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: