Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Victory Christian Center (VCC), Huruma Nkone (katikati), akizungumza katika na mkutano wa waandishi wa habari kuelezea tamasha la Campus Night linalotarajia kufanyika kuanzia kesho na hitimisho lake ni tarehe 11/11/2011. Pembeni yake ni kulia ni Samwel Sasali ambaye ni mkuu wa masuala ya habari anayesimamia tamasha hilo na Mary Kiwalaka ambaye ni mjumbe.
Samwel Sasali ambaye ni mkuu wa masuala ya
habari anayesimamia tamasha la Campus Night akizungumza kuelezea jinsi walivyojiandaa kufanya vyema katika tamsaha hilo. Katikati ni Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Victory Christian Center (VCC), Huruma
Nkone, na Mary Kiwalaka ambaye ni mjumbe.
---
UBADHIRIFU unaofanywa na baadhi ya viongozi nchini umeelezwa kuwa unatokana na kutokuwepo kwa programu ya kuwandaa kushika nyadhifa hizo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Victory Christian Center (VCC), Huruma Nkone, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa programu maalum ya kuwaandaa wanafunzi kiuongozi inajulikana kama Campus Night.
“Tunafanya programu hii kwa lengo la kuwapa elimu wanafunzi wa vyuo vikuu ya juu kuwa kiongozi bora, ili baadaye wawe viongozi wenye maadili na hofu ya Mungu ndani yao” alisema
Alisema nchi imekosa program hizo hali inayosababisha viongozi kulaumiwa pale wanapofanya makosa.
Alifafanua kwamba kunahitajika program za uongozi ili lawama zisiegemee upande mmoja wa viongozi hao.
Mchungaji Nkone alisema kwa kulitambua hilo, wameandaa program hiyo (Campus Night), ambayo itafanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni kesho jioni.
Alisema katika kufanikisha Campus Night, wanafunzi zaidi ya 15, 000 wanatarajiwa kuhudhuria bila kiingilio.
Aliongeza kuwa, wageni mbalimbali kutoka nje ya bara la Afrika watatoa mada za kiuongozi na utawala bora pamoja na elimu Kiroho.
Alisema, wanatarajia kuona Campus Night ikitoa mwanga kwa wanafunzi hao katika kuependa na kuwa wazalendo na nchi yao.
Programu hiyo, imefadhiriwa na kanisa hilo kwa kushirikiana na huduma ya Kiroho ya SOS chini ya Mchungaji Johannes Amrtzer wa Sweden.
Toa Maoni Yako:
0 comments: