Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, imemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr Jakaya Mrisho Kikwete kukutana na Vyama vyote vya Siasa vyenye Uwakilishi Bungeni ili kupanua wigo wa mawazo katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya.
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaambia Waandishi wa Habari mjini Dodoma wakati akieleza maazimio yaliyofikiwa mwishoni mwa mkutano huo wa Kamati Kuu kuhusiana na azma ya CHADEMA ya kuunda Kamati ili kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa suala la Katiba mpya.

Toa Maoni Yako:
0 comments: