Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Thomas Jilala (22), mkazi wa Kisesa mkoani Mwanza, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa akikabiliwa na mashtka mawili, likiwemo moja la kumuua mpenzi wake, Revina Ndunguru (26), wakati wakiwa katika nyumba ya kulala wageni mjini Songea, Ruvuma.
Akisoma shtaka la kwanza, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Casmili Mwalunyungu, Wakili wa Serikali, Hamimu Nkoreye, alidai kuwa Jilala alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka huu, huko katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Mikumi iliyoko mtaa wa Matomondo.
Wakili huyo, alidai kuwa Jilala alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 198 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, ambapo mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Hakimu Mwalunyungu aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 15 ambapo shauri hilo litafikishwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa na mtuhumiwa ataendelea kubaki mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika.
Katika shtaka la pili Jilala anadaiwa kuvunja na kuingia katika jengo la ofisi ya Mpenda Mvula na kuiba kompyuta aina ya dell, printer, simu moja aina ya Zain, saa moja ya mkononi na hundi namba 10553313 yenye thamani ya sh 135,000, vyote vikiwa na jumla ya sh 960,000.
Wakili Nkoreye alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka huu huko katika mtaa wa Dilux Manipsaa ya Songea. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 17.

Toa Maoni Yako:
0 comments: