katikati
ni gari ndogo nyekundu iliyokandamizwa chini ya gari kubwa jeupe la
mafuta. ambao kulikuwa na mtu ambaye alikuwa bado yupo hai na watu walikuwa atika harakati za kumuokoa. Ambapo katika ajali hiyo jumla ya watu watatu
wamelifariki pale pale kati ya hao kulikuwa na mama mjamzito ambaye kichwa na kiwiliwili vimetengana.
Baadhi ya watu katika eneo la ajali.
Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog
WATU wawili wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ajali mbaya iliyotokea jana saa saba mchana katika eneo la
Ubungo Riverside, Jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilihusisha lori la mafuta lenye namba za usajili T 269 BRQ na tela lenye namba T 264 BUC, ambalo lilikuwa likitoka Ubungo kwenda Buguruni, kuhama upande wa pili wa barabara, kugonga magari saba madogo na kuanguka.
Magari yaliyogongwa ni T 112 BTT aina ya Saloon, T 133 ADC Toyota chesar, T 918 BHC Toyota Colola, T 969 AVM Canter, T 302 AVC Pickup na T 501 BJH aina ya Noah ambayo yalikuwa yakitokea Buguruni kuelekea Ubungo.
Akizungumza na Majira, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, aliwataja waliokufa kuwa ni Bw. Venoni Sebastiani(38) mkazi wa Tabata Kinyelezi, ambaye alikanyagwa na lori hilo wakati akivuka barabara.
Kamanda Kenyela alisema, ajali hiyo pia ilisababisha kifo cha mwanamke mjamzito ambaye jina lake halijafahamika hadi sasa.
“Huyu mwanamke alikuwa akivuka barabara ndipo alipogongwa na lori, kichwa chake kilikatika na kutenganishwa kiwiliwili, rereva wa lori alikuwa akikwepa daladala iliyokuwa ikitoka kituoni wakati akiwa mwendo kasi ndio lihamaha barabara,” alisema.
Aliongeza kuwa, mama huyo alipondwa na kusagika pamoja na kichanga kilichokuwa tumboni.
Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Bw. Musa Charles (35), mkazi wa Kinondoni ambaye alikatika miguu yote miwili na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Bw. Yahaya Makame Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wengine ni Bw. Abasi Julius (24), mkazi wa mkazi wa Vingunguti na Bw. Prospa Mwakitaluma (34), mkazi wa Ubungo Changanyikeni ambao wote wamelazwa Hosptitali ya Amana.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, dereva wa gari namba T 302 AVC ambaye alinusurika katika ajali hiyo Bw. Said Sadick, alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori ambalo lilikuwa likikwepa daladala.
“Kama angeligonga daladala hilo, angesababisha vifo vya watu wengi zaidi ndio maana alichukua uamuzi wa kulikwepa, daladala husika iliondoka bila kukamatwa,” alisema.
Kwa upande wake, Dereva wa gari namba T501 BJH, ambaye alijitambulisha kwa jina moja Bi. Anna, alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa daladala ambaye alikuwa akitoka kituoni bila kuchukua tahadhari.

huyu mama aliyefariki hakuwa mjamzito nadhani kutokana na hali ya mwili wake baada ya kugongwa ndo maana imedhaniwa hivyo! tunamshrkuru Mungu tumezika salama ! polen wafiwa wengine!
ReplyDelete