Basi la kampuni ya Budget lenye namba za usajili T 207 BFJ aina ya Scania likiwa limepinduka eneo la Mlimanyoka jijini Mbeya jana.
Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabara, akikagua basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 207 BFJ mali ya kampuni ya Budget lililopinduka jana majira ya saa 12:30 asubuhi eneo la Mlimanyoka jijini Mbeya ambapo zaidi ya abiria 50 wamenusurika.

AJALI hiyo imetokea jana asubuhi baada ya basi hilo lililokuwa linaendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Bwana Mwamtobe lilipojaribu kuyakwepa maroli mawili yaliyokuwa yakipandisha katika Mlimanyoka maeneo ya Uyole jijini Mbeya.

Majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya ambapo hali zao zinaendelea vizuri, baadhi ya majeruhi ni Vumilia Maiko na Bwana Mateni Beni.

Mkuu wa usalama barabarani, Bwana Ezekiel Mgeni, amewataka madereva kuwa makini wanapoendesha magari ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Bwana Advocate Nyombi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwaasa madereva kuwa makini.

Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: