Balozi wa Hennessy Bw. Cyrille Gautier’s anaishi katika ubingwa wa dunia ya maajabu ya Hennessy nchini Ufaransa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea juu ya kinywaji cha Hennessy.
Balozi wa Hennessy Bw.Cyrille Gautier’s akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) aina ya kinywaji cha Hennessy XO kinachotengenezwa nchini Ufaransa na kusambazwa kote Afrika.
Balozi wa Hennessy Bw.Cyrille Gautier’s akikisifia kinywaji cha Hennesy aina ya XO kinachotengenezwa nchini Ufaransa.
----
Zaidi ya miaka 250 ya urithi na utaalamu wa kipekee, makazi ya Hennessy bila shaka yameweza kumudu sanaa ya kutengeneza kinywaji aina ya COGNAC. Kuanzia kwenye kulima mizabibu, kutengeneza mvinyo na mpaka kukomaa na kuzitengeneza zabibu.

Hennessy ni kinywaji aina ya COGNAC ambacho kinatengenezwa huko Cognac Ufaransa pekee. Ni kinywaji kinachotokana na aina pekee za zabibu ziitwazo Ugn Blanc ambazo ndizo zinazofaa kwa kutengeneza kinywaji hiki.

Jina la kinywaji Hennessy linatokana na mtu aliyegundua kinywaji hiki Richard Hennessy mwaka 1765. Alikuwa ni afisa kutoka kisiwa cha ireland akimtumikia mfalme wa Ufaransa na akaona kuwa kinywaji hiki kinaweza kufanya vizuri kibiashara na ndipo akaamua kuanzisha biashara yake juu ya kinywaji hiki na kuifanya kuwa biashara ya familia yake ambayo imeendelea kuendeshwa mpaka leo hii.

Kwa zaidi ya karne mbili, vizazi vinane vya familia ya Hennessy vimefanikiwa kuiendeleza biashara hii na kuzidi kukifanya kinywaji hiki kuzidi kupendwa duniani kote. Mafanikio haya yametokana na kutambulika na kuungana na makampuni mengine maarufu duniani kama Moët & Chandon champagnes mwaka 1971, pia kuungana na Louis Vuitton mwaka 1987, na bila kusahau LVMH ambao ni moja ya makundi maakubwa maarufu duniani.

Cyrille Gautier’s anaishi katika ubingwa wa duniaa ya maajabu ya Hennessy. Akiwa kama balozi wa Hennessy kwa miaka tisa iliyopita, anatembea sehemu mbalimbali duniani kuwaelezea watu juu ya mapenzi yake na uelewa wake juu ya kinywaji hiki.

Alipotembelea nchini Tanzania, Cyrille alisema “nafurahia kuwepo hapa na kuwaeleza utaalamu wangu juu ya kinywaji hiki cha Cognac na pamoja kuwajuza zaidi juu ya Hennessy. Tumejitolea kuhakikisha tunakiendeleza kinywaji cha Hennessy katika soko hili kwani tunaamini kuwa soko la Tanzania linahitaji vilivyo bora tu”

Cyrille akaongeza “Ikiwa ni sehemu ya mkakati wetu kidunia tunataka kuianzisha tamaduni Cognac, kinywaji chenye hadhi ya juu katika soko la ndani na tunaamini wateja wetu wataweza kupata ladha ya utajiri nay a daraja la juu inayopatikana katika kinywaji cha Hennessy.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: