Ikibakia kuwa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo yenye ubunifu wa hali ya juu Tanzania na ikihakikisha kutoa huduma zinazomlenga mtumiaji wa mawasiliano, Tigo inazindua Web Airtime Top-up, huduma ya kununua muda wa maongezi kwa njia ya mtandao.   

Kwa watu wenye kadi za benki za VISA kwa malipo ya baadaye sasa wanaweza kwa urahisi na kwa usalama, kuongeza salio kwa familia, marafiki na jamaa popote nchini Tanzania kwa kutumia huduma hii mpya na bunifu ya Tigo kwa njia ya mtandao kutoka sehemu yeyote ulimwenguni.

“Sisi siku zote tunahakikisha kwamba tunawapatia wateja wetu fursa ya kuchagua huduma mbali mbali," alisema Diego Gutierrez Makamu Mkurugenzi mkuu wa Tigo.  "Tunataka kupanua wigo na ufanisi katika njia za kuongeza salio kwenye mtandau wa Tigo," alisema.

WEB AIRTIME TOP-UP ni huduma ya kununua na kuongeza salio kwa njia ya mtandao kwa wateja wa Tanzania wenye akaunti zilizolipiwa kabla. Kwa kuingia kwenye mtandao wa http://topup.tigo.co.tz, wateja wanaweza kujisajili kwa kutumia jina kamili, anuani ya barua pepe, namba ya simu ya mkononi na nchi walipo.

Usajili ukikamilika wataweza kuunda kundi la marafiki yenye majina na namba za simu za watu wanaotaka kuwapelekea salio. Huduma za ziada ni pamoja na uwezo wa kutuma ujumbe wa maneno(sms) mara 5 bure kwa siku na huduma ya kutunza namba za simu za wale wanaowasiliana nao mara kwa mara.

Wateja wataonyesha kiasi cha muda wa maongezi wanaotaka kununua pamoja na taarifa zao za benki. Thamani ya vocha katika hela za kiTanzania zitathamanishwa kwenye hela za nchi inayotuma. Muda wa maongezi utakaopatikana ni TZS 5,000, TZS 10,000 na TZS 20,000. Mara makato yatakapokuwa yamekamilika salio litaingia moja kwa moja  kwa anayetumiwa, na ujumbe wa udhibitisho utatumwa ukimtambulisha pia aliyefanya manunuzi hayo.

"Huduma zetu zinapatikana masaa 24, siku 7 za wiki na malipo yote ni salama yanayo idhinishwa na VeriSign, kampuni ya mtandao inayotambulika duniani kote kwa kutunza taarifa binafsi” alisema Gutierrez. Tunafurahi kutangaza kwamba tunashirikiana pia na benki ya I & M ambao watakuwa wanaendesha shughuli zetu zote zenye kutumia mtandao," alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: